Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 2 February 2015

FAHAMU NAMNA UNAVYOWEZA KUWA NA AFYA BORA AU MBAYA KUTOKANA NA MAZINGIRA NA MPANGILIO WA MLO.Mazingira ni miogoni mwa sababu zinazoweza kumfanya mtu kuwa na afya bora au afya yenye kudorora.

Tukizungumzia mazingira tunapaswa kujiuliza kuhusu maji tunayokunywa na kutumia ni safi na salama? hewa tunayovuta si chafu? maeneo tunayofanyia kazi ni salama? na pia nyumba tunazoishi zipo katika mazingira yapi? Lakini kama yote hayo yatakuwa yapo vizuri basi afya zetu zina asilimia kubwa ya kuwa salama zaidi ikilinganishwa na watu wanaoishi kwenye maeneo yasiyo na maji safi na salama au kuvuta hewa chafu na kufanya kazi kwenye mazingira ya hatari.

Kuna uchunguzi uliowahi kufanywa na Chuo Kikuu cha Zuyd kilichopo nchini Uholanzi na ulibainisha kwamba, kuvuta hewa iliyochafuliwa kwa gesi za magari kwa saa moja hutosha kumsababishia mtu mfadhaiko wa kifikra au ‘stress’ katika ubongo wake.

Aidha, afya ya binadamu pia huweza kuathiriwa na watu wanaomzunguka. Mfano ikiwa wewe unaishi na familia karibu au marafiki katika jamii yako, basi una nafasi kubwa ya kuimarisha afya yako kuliko mtu ambaye anaishi peke yake au hana familia na marafiki.

Kwa mujibu wa uchunguzi uliowahi kufanywa na Chuo Kikuu cha Washington nchini Marekani waligundua kuwa, ushirikiano wa kifamilia ni jambo zuri kwa mtu na hupunguza hata uwezekano wa matukio ya kujiua, hususani kwa wale wanaopatwa  na matatizo ya mfadhaiko wa kifikra au wanapokuwa na fikra ya kutaka kujiua.

Suala jingine linaloweza kuchangia uwepo wa afya bora kwa jamii ni kuhusu matumizi ya vituo vya afya na hospitali. Jamii ambayo ina vituo vya afya vya kutosha, vilivyo vizuri na vyenye kukidhi mahitaji ya watu wa jamii hiyo, mara zote watu wake watakuwa katika nafasi kubwa ya kuwa na afya bora kuliko jamii au watu wanaoishi maeneo ambayo hayana vituo vya afya au hospitali.

Mfano mzuri ni katika nchi zilizoendelea na zenye vituo vya afya na hospitali za kutosha na nzuri, mara nyingi watu wa nchi hizo huishi maisha marefu zaidi ikilinganishwa na nchi masikini ambazo zinaupungufu katika sekta hiyo.

Miongoni mwa mambo muhimu yanayoijenga afya ya mwanadamu ni kula lishe bora na mlo uliokamilika. Lishe bora na mlo uliokamilika hii huwa na maana ya kwamba ni kula kwa kiwango kinachotakiwa kulingana na mahitaji ya mwili wako, pia kula aina tofauti za vyakula vinavyotakiwa ili kuijenga siha ya mwili.

Tunapaswa kufahamu kwamba, kula lishe bora ni suala muhimu linalochangia kuimarisha afya ya mwili. Lishe salama na iliyokamilika inamaanisha kula vyakula tofauti kutoka katika mafungu manne makuu ya vyakula na kupunguza baadhi ya vyakula katika milo tunayokula kila siku.

Ifahamike kuwa aina ya vyakula tunavyopaswa kuwepo kwenye milo yetu ni pamoja na matunda na mboga kwa wingi.  Kiwango cha kutosha cha wanga kama vile wali, viazi, mkate na vingine, lakini ni bora viwe vinatokana na aina mbalimbali za nafaka kamili zisiokobolewa.
Sambamba na maziwa na vyakula vinavyotokana na maziwa kama mtindi na jibini. Vyakula vyenye protini kama samaki, mayai, nyama, maharagwe na vinginevyo ikiwa ni pamoja na kiasi kidogo sana cha na sukari, mafuta na chumvi.

Pamoja na hayo ni vizuri kuzingatia kuwa, mlo tunaokula uwe na kiasi cha kutosha cha wanga, kwani aina hiyo ya chakula huipa miili yetu nguvu pamoja na kula matunda na mboga kwa wingi kila siku.

Pia ni vizuri kupunguza matumizi ya sukari na mafuta katika milo yetu. Vilevile ni vizuri kula chumvi kwa kiwango kidogo. Hii ni kwa sababu ongezeko la chumvi mwilini huweza kumfanya mtu apatwe na shinikizo la damu, hali ambayo huweza kusababisha ugonjwa wa moyo na kiharusi.

Suala jingine tunalopaswa kuzingatia ni kunywa maji ya kutosha, tunashauriwa kila siku kunywa kiasi cha glasi 6 hadi 8 za maji au vyakula vingine vya majimaji kama juisi na kadhalika, hii husaidi upungufu wa maji mwilini. Tambua kuwa maji yana faida nyingi ikiwa ni pamoja na kuusaidia mwili kuondoa kwa urahisi sumu na mabaki yasiyotakiwa mwilini.

Hayo ndiyo baadhi ya mambo ya msingi yanayoweza kukuacha ukiwa mwenye afya siku zote.Tunapenda kukukaribisha kuanza kutangaza nasi kupitia tovuti hii ambayo inatembelewa na watu wengi kwa sasa, unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0758 163 818 / 0672 060 0006 au Barua pepe: dkmandaitz@gmail.com gharama zetu ni nafuu sana. Karibu!!

No comments:

Post a Comment