Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 16 February 2015

FAHAMU UWEZO HUU MWINGINE WA NAZI KATIKA KUONDOA VIPELE VYA JOTO MWILINI
Upele wa joto hutokana na kutoa jasho jingi kuliko kiasi na kuanza kufanya mwili uanze kuwasha washa. 


Tatizo hili huwapata zaidi watu wanaoishi mjini na kujishehenesha katika kuvaa na kuishi katika nyumba zilizosongamana zisizo na uhuru wa mzunguko wa hewa.

Mara nyingi tatizo hili huonekana kuwa ni dogo kwa wengine, lakini tatizo hili ni kubwa na huwakosesha raha hasa kwa watoto.
 
Mtaalam wa tiba asili kutoka Mandai Herbalist Clinic, Dk Abdallah Mandai anasema kuwa tui la nazi  linauwezo mkubwa wa kutatua tatizo hili.

Mtaalam huyo anaeleza kuwa unapohitaji kutumia tui la nazi kumaliza tatizo hili la vipele vya joto kwanza unapaswa kukuna nazi moja kubwa kiasi, kisha changanya glasi moja ya maji na ukoroge vizuri na uchuje ili ubaki na tui lililo safi.
 
Baada ya hapo Dk Mandai, anasema mchanganyiko huo utapaswa kupakwa mwili mzima wenye tatizo na mara baada ya saa moja mhusika atatakiwa kuoga kwa maji ya baridi.Tumia tiba hiyo mara kadhaa na itasaidia kumaliza tatizo hilo.

Anza sasa kutangaza na tovuti hii kwa gharama nafuu sana, tunapokea matangazo ya aina yoyote unachopaswa kufanya ni kuwasiliana nasi kwa namba za simu hizi zifuatazo, 0672 060 006, 0758 163 818, au Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment