Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 23 February 2015

FAHAMU VYAKULA VINAVYOWEZA KUIMARISHA AFYA YAKO YA NGOZINgozi nayo ni sehemu muhimu ya mwili ambayo ina jukumu kubwa la kuukinga na kuufunika mwili na viungo mbalimbali,
hivyo ni vizuri afya ya ngozi ikazingatiwa.
Aina ya vyakula tunavyokula vinauwezo mkubwa kuchangia muonekano mzuri wa ngozi zetu na kusaidia kupambana na matatizo ya ngozi ikiwa ni pamoja na kupunguza mikunjano ya uso na suala zima la afya na muonekano wa ngozi.

Ni wazi kwamba wengi wetu tunapenda kuonekana vijana na warembo, lakini kwa sababu ya kutofahamu njia sahihi za kudumisha ubora wa ngozi huenda ikawa sababu ya kufanya wengi tusifikie lengo hilo na hata kusababisha kupata madhara yasiyotibika kwa baadaye.

Huenda umekuwa ukitumia fedha nyingi katika kuhakikisha ngozi inakuwa nzuri na ya kuvutia, lakini huenda ukawa haufahamu kuwa kuna baadhi ya aina fulani ya vyakula ambavyo vinaweza kutunza ngozi yako na tena bila gharama kubwa.

Wataalam wa masuala ya lishe wanasema kuwa kila ambacho tunakula huwa kinakuwa ni sehemu ya mwili wetu ikiwa ni pamoja na sehemu ya nje na kwamba, kila tunavyokula vyakula bora ndivyo ngozi inavyozidi kupata muonekano vizuri.

Vifuatavyo ni vyakula vinavyoweza kusaidia kuimarisha afya ya ngozi:-

Asali ambayo hutengenezwa na nyuki kwa viambato asilia ni chakula muhimu kwa ajili ya kuimarisha afya ya ngozi na pia afya ya binadamu. Asali husaidia kutunza na kuhifadhi unyevu kwenye ngozi na ina kiwango kikubwa cha sukari na asidi ambazo huzuia vijidudu wanaozaliana kwenye ngozi.


Unapohitaji kulinda ngozi kwa njia hii, paka asali wakati wa kuoga, acha kwa muda kisha ioshe. Kufanya hivyo kunaweza kuinawirisha ngozi yako.

Vyakula vya baharini ni vizuri pia kwa afya ya ngozi, kutokana na vykula hivyo kuwa na kiwango kikubwa cha zinc na Omega 3 ambazo ni muhimu kwa afya ya ngozi. 

Faida za Omega 3 ni pamoja na kuondoa kukakamaa au ukavu wa ngozi, kupunguza kuvimba na kukunjamana kwa ngozi na husaidia mzunguko mzuri wa damu mwilini hivyo kuboresha ngozi. 

Damu inapozunguka vyema mwilini afya ya ngozi hayo huimarika. Hii ni katika hali ambayo zinc husaidia kuondoa chunusi na harara katika ngozi kwa kuyeyusha homoni ya testosterone. Pia husaidia kuzalishwa seli au chembe hai za mwili na kuondoa chembe zilizokufa huku ikiifanya ngozi ing'ae na kuwa na mvuto.
Ngozi ya mwanadada inayoonekana kuwa na afya
Chakula kingine muhimu kwa ajili ya kuimarisha ngozi ni mayai, yai ni kirutubisho muhimu kwa afya kwani lina virutubisho muhimu sana kwa afya ya ngozi. Kiini cha yai kina vitamini A na B, huku sehemu yenye ute ikiwa na protini nyingi ambayo ni muhimu pia kwa ngozi.

Matunda yenye vitamini C kama vile chungwa, limao na mengineyo ni muhimu pia katika kuimarisha afya ya ngozi, kwa sababu husaida kutengeneza collagen, ambayo ni aina ya protini inayotengeneza ngozi.  Vilevile vitamini C inasaidia kuondoa uvimbe na mikunjo ya ngozi na hivyo kuilinda ngozi isizeeke mapema. 

Mboga za majani pia ni muhimu kwa afya ya ngozi kama tujuavyo zimesheheni vitamin na virutubisho vya aina mbalimbali vyenye faida kubwa kwa ngozi na mwili kwa ujumla.

Hali kadhalika karanga na vyakula jamii ya karanga vina vitamin E, ambayo ni muhimu katika kuzuia kuzeeka kwa ngozi hasa kutokana na kupigwa sana na jua.
Vyakula ambavyo vinauwezo wa kuimarisha afya ya ngozi ni vingi, lakini kunywa maji kwa wingi nako ni muhimu ili kuifanya ngozi iwe nyororo.

Endapo unasumbuliwa na magonjwa sugu basi wasiliana na Mandai Herbal Clinic kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.  

No comments:

Post a Comment