Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 6 February 2015

FAIDA ZA BAMIA MWILINI
Unaweza kupata faida nyingi endapo utakula bamia na ukawa katika nafasi kubwa ya kujiondolea uwezekano wa kupata maradhi hatari mbalimbali.


Kwa mujibu wa mtandao wa healthandcure.com uliwahi kuwanukuu baadhi ya wataalam wa afya wakieleza kwamba watu wanaosumbuliwa na maradhi ya mfumo wa chakula kama vile vidonda vya tumbo na mengine yanayofana na hayo wanaweza kupata ahuweni au kupona kabisa ikiwa watakula bamia.

Aidha, faida nyingine zinazotokana na ulaji wa bamia ni pamoja na kuwa chanzo kizuri cha vitamin A, lakini pia husaidia kuboresha uwezo wa macho kuona.

Pia bamia inasaidia kuweka kawaida kiwango cha sukari mwilini, huku nyuzinyuzi zake zikielezwa kurahisisha ufyonzwaji wa sukari mwilini. Pia hudhibiti pia kiwango cha lehemu mwilini na hasa pale inapokuwa mtu ametumia vyakula vingi vyenye mafuta.
Bamia ikiwa katika mmea wake
 Mbali na hayo, pia husaidia kulainisha choo na huwasaidia baadhi ya watu ambao hukosa hamu ya kula, pia husaidia kurahisha kumeza. 

Pamoja na haya, yote bamia huimarisha mifupa, huongeza kinga dhidi ya magonjwa ya figo, saratani pamoja na pumu.

Pia unaweza kufika Mandai Herbalist Clinic nakupata tiba ya magonjwa mbalimbali, kituo kipo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.

1 comment:

  1. nasikia sio mzuri kwa wananaume zinapunguza nguvu za kiume ni kweli

    ReplyDelete