Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 14 February 2015

FAIDA ZA HIRIKI KATIKA TIBA
Hiriki ni mmea mfupi wa takribani mita 1 hadi 3 mfano wa mgomba kwa mbali mbegu zake hota chini mwanzoni mwa shina kama mizizi ya juu isipokuwa huwa ba mizizi ya juu  na ina mbegu.


Tiba za hiriki ni pamoja na kutoa gesi tumboni, kusaidia kukabiliana na tatizo la usagaji wa chakula pamoja na kuondoa tatizo la maumivu au mvurugiko wa tumbo.

Pia husaidia kuleta hamu ya kula kwa wale ambao hukosa hamu ya kula, lakini pia husaidia kuondoa unene kwa wale wenye miili mikubwa.

Mbali na magonjwa hayo, pia hiriki hutibu matatizo ya meno na fizi unapotafuna, na kwa wale wenye shida ya mapafu kubana basi huweza kuwa msaada mkubwa kwa shida hiyo.

Hizo ni faida chache za hiriki tafadhali endelea kutembelea tovuti hii kwa kujua mambo mengi zaidi kuhusu mimea tiba kama hii. Pia unaweza fika Mandai Herbalist Clinic iliyopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. Au piga simu namba
0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443


No comments:

Post a Comment