Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 4 February 2015

FAIDA ZA MATUMIZI YA MAFUTA YA NAZINazi ni kiungo kizuri ambacho hutumika kuongeza uzuri wa vyakula jikoni, lakini pia kiungo hiki  ndani yake kuna asidi muhimu kwa afya ya moyo ambayo inaitwa ‘lauric acid’ . Asidi hiyo huongeza uwepo wa kolesteroli nzuri mwilini ijulikanayo kwa kitaalam kama High Density Lipoprotein (HDL), ambayo husaidia kuishusha ile kolesteroli mbaya ijulikanayo pia kwa kitaalamu kama Low Density Lipoprotein (LDL) jambo ambalo ni mhimu kwa afya ya moyo.

Dk Abdallah Mandai anasema kuwa nazi inafaida nyingi kwa afya endapo itatumiwa ipasavyo, miongoni mwa faida hizo ni pamoja na kusaidia kuongezea nguvu mfumo wa mmmeng’enyo wa chakula, kwa hili hutumika zaidi mafuta ya nazi.
 

Pia mtaalam huyo anasema kuwa nazi husaidia kuimarisha utumbo, hufanya viungo kuwa na nguvu, husaidia upungufu wa uzito, pamoja na kuondoa uchovu mwilini.

Nazi pia husaidia kuimarisha afya ya ngozi, kama unataka kuwa na ngozi nzuri yenye mng’aro na yenye afya na yenye muonekano wa asili basi paka mafuta ya nazi kila siku kwenye ngozi yako, mafuta ya nazi yana uwezo mkubwa katika kuua bakteria, virusi, na vijidudu vya aina yeyote vinavyoweza kuidhuru ngozi yako.

Kutokana na uwepo wa kiasi kingi cha asidi ya ‘lauric acid,’ huyafanya mafuta ya nazi kuendelea kuwa na uwezo mkubwa wa kupambana na maradhi mengine hatari mwilini.
 
Faida ni nyingi za nazi na hizo ni baadhi tu ya zile nyingi, lakini zingatia kuwa unahakikisha unapata mafuta ya nazi ambayo ni ya asili kwa asilimia 100, kwani endapo utanunua dukani huenda yakawa yamechanganywa na kemikali nyingine.

Unaweza kufika Mandai Herbalist Clinic kwa huduma mbalimbali za kiafya, kituo kipo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment