Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 9 February 2015

FURSA YAKO YA KUELEWA NAMNA BAKTERIA WA KIPINDUPINDU WANAVYOINGIA MWILNI NA KUANZA KUSHAMBULIA
Ugonjwa wa kipindupindu ni ugonjwa ambao hutokana na maambukizi katika utumbo mdogo wa binadamu ambayo husababishwa na vimelea vya bacteria wajulikanao kitaalam kama Vibrio Cholerae.


Mara nyingi vimelea hao wanaosababisha kipindupindu hupendelea kuishi katika kinyesi cha binadamu , hivyo mtu anaweza kuambukizwa ugonjwa huu kwa kunywa maji ya au chakula kilichochanganyikana na kinyesi chenye vimelea hivyo vya kipindupindu.

Vimelea hivyo vinapoingia tumboni mwa binadamu baadhi yao hufanikiwa kuuwawa na tindikali iliyopo tumboni, lakini baadhi ya vimelea hufanikiwa kukwepa ukali wa tindikali hiyo na hivyo kuendelea kuishi.

Vimelea wanaokuwa wamefanikiwa kukwepa tindikali hiyo huanza kujongea kwenda kwenye ukuta wa utumbo mdogo kwa kutumia maumbo maalum na wanapofika kwenye ukuta wa utumbo mdogo vibrio cholerae huanza kutoa sumu iitwayo CTX  au CT (cholerae toxin) ambayo huanza kusababisha mtu kuharisha  choo chenye majimaji.

Wakati huo muathirika akianza kuharisha choo cha aina hiyo huweza kutokea mlipuko wa ugonjwa huo zaidi endapo choo kitachanganyika na chanzocha maji au chakula na hapo ndipo watu wengi huanza kuambukizwa kirahisi.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO),kunamakadirio kuwa matukio milioni 3 hadi 5 na vifo 100,000 hadi 120,000 kiala mwaka kutokana na ugonjwa wa kipindupindu duniani kote, huku watu wenye kinga hafifi za mwili kama waathiria wa HIV huweza kuwa katika hatari ya kupoteza maisha zaidi pindi wakipata ugonjwa huu.
Mnamo mwaka 2000, wagonjwa 14,000 waliripotiwa kuugua kutokana na kipindupindu, huku takribani asilimia 87 waliripotiwa walikuwa ni kutoka barani Afrika.

Miongoni mwa dalili za ugonjwa huu ni pamoja na  mgonjwa kuanza kuahrisha ghafla choo chenye majimaji (ambacho maji yake ni kama maji ya mchele) na kuambatana na harufu mbaya.

Aidha, mgonjwa hutapika na huwa na dalili za kupungukiwa maji mwilini kama vile ngozi kuwa kavu, midomo kukauka, mgonjwa kuhisi kiu sana, kuapata mkojo kidogo sana, machozi kuacha kutoka, kuishiwa nguvu na kujisikia uchovu sana, macho kutumbukia ndani hasa kwa watoto.

Njia kuu itumikazo katika kumrejeshea mgonjwa wa kipindupindu maji na maddini aliyopoteza ni kwa kumpatia maji maalum yenye madini hayo kwa njia yam domo, yaani kwa kumpa anywe au kwa njia ya mishipa ya damu ambayo kitaalam huitwai 'intravenously' .

Hata hivyo, mara nyingi serikali na taasisi zake imekuwa ikihamasisha wananchi jinsi ya kujikinga na ugonjwa huu na miongoni mwa mbinu ambazo zimekuwa zikitolewa ni pamoja na kuwahamasisha watu kutumia maji ya kunywa yaliyochemshwa vizuri kabla ya kunywa, kunawa mikono baada ya kutoka chooni na kabla ya kula, kufunika vyakula vizuri ili visifikiwe na nzi na inashauriwa kujenga choo angalau mita 30 kutoka chanzo cha maji.

Pia kuosha matunda  na kumenya kabla ya kula, vifaa vyote vinavyotumiwa na wagonjwa vinapaswa kuchemshwa kwa maji ya moto pamoja na mashimo ya choo yanapaswa kutiwa dawa za kuua bakteria kwa kutumia ' klorini'.

No comments:

Post a Comment