Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 26 February 2015

HAYA NDIYO YALIYOENDELEA KUHUSU MWALIMU AMBAYE ALIAMUA KUISHI NA KINYESI CHUMBANI KWAKE
Manispaa ya Temeke Dar es Salaam  hapo jana ilifikia uamuzi wa kubomoa mlango wa chumba cha mwalimu  Gaudensia Albertwa, ambaye anafundisha Shule ya Sekondari Kibasila
kwa lengo la kumwaga kinyesi alichokuwa amehifadhi kwa miaka miwili.

Zoezi hilo la kumwaga uchafu huo uliokuwa umechanganyikana na kinyesi, mkojo na matapishi na ulikuwa umehifadhiwa kwenye ndoo kubwa na ndogo, sufuria  kubwa na ndogo, beseni makubwa na madogo pamoja na chupa za soda na maji.

Mbali na uchafu huo katika chumba cha mwalimu huyo, pia kulikuwa na wadudu wa aina mbalimbali wakiwemo mende na funza wakubwa wakiwa wamezagaa sakafuni na kitandani.

Maofisa wa Manispaa ya Temeke walitumia zaidi ya dakika 20 katika zoezi hilo la umwagaji wa kinyesi hicho na baada ya kumaliza walilazimika kusafisha chumba hicho cha mwalimu.

Kinyesi hicho kilitupwa kwenye mashimo ya kuhifadhia maji taka yaliyokuwa kwenye eneo la nyumba hiyo.

Baada ya kumalizika kwa zoezi la umwagaji wa uchafu huo, diwani wa kata hiyo Abel Tarimo alisema kutokana na tukio hilo ambalo si la kawaida zitafuatwa sheria mbalimbali za mazingira ili kuweza kumchukulia hatua mwalimu huyo.

“Hili si tukio la kawaida, hivyo kwa sasa mimi kwa kushirikiana na viongozi wa ngazi mbalimbali tutajipanga kufanya msako kwa kila nyumba na endapo mtu wa aina hiyo tutawachukulia hatua.”

Naye Ofisa Afya na Usafi wa Mazingira katika Manispaa hiyo, Jumanne Muhongo alisema tukio hilo ni la kipekee na kihistoria kwani halikuwahi kutokea katika wilaya hiyo.

Aidha alifafanua kuwa hadi sasa halmashauri hiyo imekutana na walimu wa shule hiyo anayofundisha mwalimu huyo na kukubaliana kumfikisha hospitali kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi zaidi kwani inasemekana huenda hana akili nzuri.

Akielezea kuhusu suala la kisheria ya mazingira, alisema kisheria mtu yeyote haruhusiwi kukaa na uchafu kiasi hicho, hivyo endapo hatua mbalimbali akifuatwa ataweza kufikishwa mahakamani kustakiwa kwa mujibu wa vifungu mbalimbali vya sheria.

“Kwa mujibu wa wa sheria ya mazingira mtu akikutwa na uchafu kama huu anafikishwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka” alisema 


Sasa tupo tayari kuanza kupokea matangazo ya biashara yako yoyote na kukuwekea kwenye tovuti hii inayotembelewa na maelfu ya watu. Karibu sana gharama zetu ni nafuu sana piga simu namba 0758 163 818, 0672 060 006, Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com


No comments:

Post a Comment