Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 16 February 2015

HEBU FAHAMU SABABU HII NYINGINE INAYOCHANGIA VIJANA KUPATA MAGONJWA YA ZINAA
Maafisa wa afya katika Ufalme wa Thai wamesema kuwa magonjwa ya zinaa miongoni mwa wavulana wa miaka 10 hadi 19 yameongezeka mara tano zaidi katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.


Maafisa hao wamesema kuwa moja ya sababu inayochangia kuongezeka kwa magonjwa hayo ni wavulana kuogopa kuchagua mipira ya kondomu zinazowatosha vizuri.

''Ni kwa sababu ni asilimia 43 ya vijana ndio wanaotumia mipira ya kondomu na kwamba huchagua mipira ambayo ni mikubwa ikilinganishwa na vipimo vyao huku wakiogopa kwamba watafanyiwa masikhara kwa kuwa wadogo''.

Hayo yalibainishwa katika taarifa ilioambatana na siku ya wapendanao yaani Valentine Day, siku ambayo maafisa wa Thai hutoa onyo kuhusu mapenzi ya ujana.


Wizara ya Afya ya Umma nchini humo imesema kwamba, inapanga kutumia dola millioni 1.4 mwaka huu ili kugawanya zaidi ya mipira milioni 43 kwa watu wote katika ufalme huo.
Afisa wa kampuni ya kutengeza mipira ya kondomu katika Ufalme wa Thai akagua mipira hiyo


Hata hivyo, taarifa zinaseleza kuwa mara nyingi vijana katika ufalme huo hufunzwa zaidi kutofanya ngono, badala kuambiwa watumie kinga wakati wanapotekeleza tendo hilo.

Chanzo: BBC Swahili.


No comments:

Post a Comment