Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Sunday, 8 February 2015

HIVI ULIKUWA UNAJUA TAKWIMU HIZI KUHUSU MATUMIZI YA POMBE?


Tumia nafasi hii leo kujua takwimu hizi kuhusu matumizi ya vileo (pombe) na namna yanavyochangia katika kusababisha vifo duniani kote.


Inaelezwa kuwa watu milioni 3.3 duniani kote hupoteza maisha yao kila mwaka kutokana na matumizi ya pombe kupita kiasi, ambapo idadi hiyo ni sawa na asilimia 6 ya vifo vyote duniani.

Makundi ambayo yanaelezwa kuwa na matumizi ya pombe kupita kiasi ni wale wenye umri wa kuanzia miaka 20 hadi 30, ambapo asilimia 25 ya vifo vyote vya watu walio katika kundi hilo hutokea kutokana na matumizi ya pombe.

Pia matumizi yapombe yanaelezwa kuchangia sana kuvuruga mahusiano ya kifamilia, ndugu, kikazi lakini pia ni moja ya chanzo cha magonjwa.

Pombe ni hatari kwa afya yako hivyo ni vizuri ukaepukana na matumizi mabaya ya pombe.

SOURCE: World Health Organization (WHO)

No comments:

Post a Comment