Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 25 February 2015

IFAHAMU NJIA HII YA KUZUIA UVIMBE UNAPOKUWA UMEUMIA, UMETEGUKA AU KUSHTUKA
Ni mara ngapi umewahi kuumia, kuteguka au kushtuka baadhi ya sehemu za mwili hasa mkono au mguu na ukajikuta sehemu uliyoumia ikivimba kadri muda unavyozidi kwenda?

Ni wazi kwamba wengi wetu tumewahi kujikuta katika hali kama hiyo ya kuumia na kujikuta sehemu tunazoumia zikivimba na wengi tunapoona hivyo tumekuwa tukitumia maji ya moto pamoja na chumvi kwa ajili ya kujikanda ili kuondokana na matatizo hayo.

Leo hii Mandai Herbal Clinic kupitia kwa Mkurugenzi Mkuu wake Dk Abdallah Mandai anakusogezea njia hii nyingine itakayoweza kukusaidia kupunguza uvimbe mara unapokuwa umeumia.

Dkt Mandai anasema kuwa, ukwaju na chumvi ni moja ya tiba nzuri ya tatizo hilo, ambapo anabainisha kuwa kinachohitajika ni kukamua ukwaju na upate juisi yake, ongeza chumvi, kisha koroga vizuri mchanganyiko huo.

Baada ya hapo mtaalam huyo anafafanua kuwa, utapaka uji huo katika sehemu zote zenye uvimbe unaotokana na kuumia/ kuteguka kisha acha uji ukauke hapo hapo na baada ya masaa 12 paka tena. 
Ukwaju
Chumvi

Endelea na zoezi hilo hadi pale uvimbe utakapokuwa umepungua.

Hiyo ni njia ambayo inaweza kukusaidia kuondokana na shida hiyo ya uvimbe ulitokana na kuumia, lakini endapo unasumbuliwa na magonjwa sugu unaweza kuonana na Dk Abdallah Mandai ambao anapatikana Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. Au piga simu namba 0758 163 818, 0672 060 006, Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com 

No comments:

Post a Comment