Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 4 February 2015

IKIWA LEO NI SIKU YA SARATANI DUNIANI, NI VYEMA UKAFAHAMU UNDANI WA UGONJWA HUO
Kansa au saratani ni kundi la magonjwa yanayosababishwa na mgawanyiko usio sawa na usiodhibitika wa seli na kuunda uvimbe unaovamia na kuzidhuru tishu. 

Kuna aina zaidi ya 100 za kansa kwa kuzingatia ni kiungo gani cha mwili kimeathirika. Hata hivyo, aina zote hizo za kensa zina sifa 3 zinazofanana ambazo ni u3ukuaji usiodhibitika wa seli, uwezo wa kuvamia na kushambulia tishu nyingine na uwezo wa kusambaa katika viungo vingine mwilini kupitia mishipa ya damu.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) wanasema kwamba, kwa mwaka 2012  saratani iliyokuwa ikiongoza kwa kusababisha vifo vya watu wengi duniani namba moja ilikuwa ni saratani ya mapafu (vifo milioni 1.59), mbili ni saratani ya ini (vifo 745 000) na tatu ni saratani ya tumbo (vifo 723 000). 

Kansa isipotibiwa inaweza kuwa ni ugonjwa unaoshambulia tishu nyingine mwilini na kusabisha kifo, kwani huusababishia mwili madhara pale inapoharibu seli na kuzifanya zigawanyike bila kudhibitika na kuwa uvimbe wa tishu unaojulikana kama tumor, isipokuwa katika saratani ya damu ambapo kansa huzuia utendaji wa kawadia wa damu kwa kuzifanya seli ziwe na mgawanyiko usio wa kawaida katika damu.

Mwili wa binadamu umeundwa kwa trilioni ya seli ambazo hukuwa, kugawanyika na kufa kwa mpangilio maalum. Mwenendo huo ulioratibiwa vyema unasimamiwa na vinasaba au DNA vilivyo ndani ya seli, lakini wakati mtu anapokuwa mtoto mdogo au ndani ya tumbo la mama, seli hujigawanya kwa haraka ili kumfanya akue. Baada ya mtu kukua, seli nyingi hugawanyika kwa ajili ya kuchukua nafasi ya zile zilizozeeka na kufa au kwa ajili ya kukarabati majeraha.

Chanzo cha saratani huanza wakati seli katika sehemu mojawapo ya mwili zinapoanza kukua bila kudhibitiwa. Hapo ndipo ukuaji wa seli za kansa ambapo hutofautiana na ukuaji wa kawaida wa seli za mwili, na badala ya kufa pale zinapozeeka zenyewe huendelea kukua na kuzaa seli nyingine mpya zisizokuwa za kawaida.

Seli za satarani pia hushambulia kwa kuingia ndani ya tishu nyingine jambo ambalo huwa halijitokezi katika seli za kawaida. Kukua kusikodhibitiwa na kusiko kwa kawaida kwa seli na tabia ya kuzishambulia tishu nyingine ndiko husababisha seli za zinazopelekea mhusika kupata kansa.

Kutokana na madhara ya ugonjwa huu na ikiwa leo Dunia inaadhimisha siku ya Saratani Duniani Dk Harrison Chuwa aliwataka Watanzania kujenga utamaduni wa kula vyakula vya asili kwa lengo la kujikinga na ugonjwa wa saratani, ambao umeonekana kuwa tishio duniani.

Akizungumza jijini Dar es Salaam daktari huyo bingwa wa magonjwa ya saratani wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk Harrison Chuwa, alisema katika kipindi cha mwaka mmoja hali ya ugonjwa huo imezidi kuwa mbaya.

Dk Chuwa, alisema hali imekuwa ikibadilika na katika kipindi cha miaka mitatu, taasisi hiyo imekuwa ikipokea wagonjwa wa saratani 1500 hadi 4000 kwa mwaka.

Aidha, alisema kati ya wagonjwa hao wengi wao ni wale ambao ugonjwa huwa umefika katika hatua ya juu kiasi cha kuchangia matibabu kuwa ya gharama kubwa.

Hali kadhalika, Dk Chuwa alibainisha kuwa, hali ya maisha ikiwa ni pamoja na namna tunavyokula imekuwa moja ya sababu ya kuchangia ugonjwa huu kwa kiasi kikubwa.

“Kuacha kula vyakula vya asili na mboga za majani ni tatizo kwani badla yake vyakula vya kemikali nyingi vimechukuwa nafasi jambo ambalo si nzuri kwa afya ya Watanzania,” alisema Dk Chuwa.

Pia alisema zipo njia nyingi za kuzuia saratani ikiwa ni pamoja na ulaji wa vyakula vya asili, hasa ugali wa dona ulioandaliwa vizuri, sambamba na kufanya mazoezi.

Dk Chuwa alifafanua kwamba kwa mujibu wa Taasisi ya Global Cane, hadi kufikkia mwaka 2012 iliripotiwa kuwapo wagonjwa wapatao milioni 14.1 duniani, kati ya hao milioni 8.2 walifariki dunia.

Mbali na hayo, Dk Chuwa aliongeza kuwa “tatizo la nchi nyingi za Afrika niuelewa mdogo juu ya ugonjwa huu, ndiyo maana wengi wanakuja wakiwa wamechelewa.”
Hata hivyo, licha ya hayo Shirika la Afya Duniani (WHO) inakadiriwa kuwa miaka 20 ijayo ongezeko la ugonjwa huo litaongezeka na kufikia kiwango cha asilimia 70.

Ikiwa unasumbuliwa na magonjwa sugu unaweza kufika kliniki ya Mandai Herbalist Clinic kituo kilichopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na utapata ufumbuzi wa magonjwa hayo.No comments:

Post a Comment