Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 3 February 2015

JAMII BADO HAINA UFAHAMU WA KUTOSHA KUHUSU UMUHIMU WA MATUNDAJamii ya Watanzania walio wengi imeonekana kutokuwa na uelewa wa kutosha kuhusu umuhimu na faida za matunda kwa afya na badala yake wengi wanasema kuwa huwa wanakula matunda mbalimbali kwa lengo la kupata shibe tu na si vinginevyo.

Hayo yamebainika jana Februari 2 baada ya timu ya tovuti hii ya www.dkmandai.com kuamua kutembelea maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na Soko la Ilala na Gongo la Mboto, Mzambarauni na kukutana na wananchi mbalimbali wakiwemo wafanyabishara wa matunda, ambao nao licha ya kuuza matunda lakini walikiri kutojua faidia za matunda kwa afya zao.

Mmoja wa wanyabiashara wa soko la Mzambarauni Gongo la Mboto aitwaye Vitalis Lazaro Kisinga, alipoulizwa juu ya faida za ulaji wa matunda alifunguka akisema kuwa “kwa kweli mimi najua faida ya matunda ni kula na kushiba tu, lakini undani wake zaidi sifahamu.”

Aidha, mbali na hayo baadhi yao walionekana kulipenda zaidi tunda aina ya parachichi na kulielezea kama tunda ambalo kila wanapokula huwa wakihisi limesheheni virutubisho vingi zaidi kutokana na namna linavyoonekana.

“Kwa sasa nina miaka zaidi ya mitano tangu nilipoanza kula parachichi, lakini ninachojua na kuamini kuhusu tunda hili ni kwamba husaidia mwili kuwa laini na linafanya ngozi inakuwa ‘soft’ sana,” alisema Baraka Rashid ambaye ni mfanyabiashara wa sokoni pia.

Kutokana na hali hiyo hapa  tovuti hii ya www.dkmandai.com inakukutanisha na Dk Abdallah Mandai kutoka Mandai Herbalist Clinic na anafafanua kuhusu faida za matunda katika miili yetu, ambapo anaanza kwa kusema kuwa “zipo faida mbalimbali za ulaji wa matunda ukiachilia mbali ladha yake, kwani matunda yana virutubisho vingi, vitamini za aina mbalimbali ambazo hupatikana kwenye matunda.”

Pia Dk Mandai anaendelea kueleza kuwa, matunda husaidia kupunguza matatizo ya moyo, kiharusi, shinikizo la damu, lehemu na aina mbalimbali za saratani pamoja na matatizo ya uwezo wa macho kuona na mengine mengi.

Mtaalam huyo pia analielezea tunda la parachichi ambalo wanachi wengi wameonekana kutofahamu faida zake ambapo anasema kuwa, pamoja na faida nyingi za parachichi, lakini pia ni tunda ambalo lina vitamini E ambayo faida yake ni kupunguza kiwango cha lehemu ‘cholesterol’ mwilini, hivyo hufanya moyo kuwa na afya njema.

Mbali na hayo, Dk Mandai anasema, ndizi ina vitamini B6 na madini ya ‘potassium,’ huku akisema kwamba kuwepo kwa madini hayo ya ‘potassium’ kwenye ndizi kumelifanya tunda hilo kuwa na uwezo wa kupunguza ongezeko la shinikizo la damu.

Nimekuwekea hapa picha za baadhi ya wafanyabiashara waliopata fursa ya kuzungumza na www.dkmandai.com kuhusu umuhimu wa matunda katika masuala ya afya.
Jeremiah Boniphac mfanyabiashara wa matunda kutoka Soko la Ilala jijini Dar es Salaam


Baraka Rashidi mfanyabiashara wa soko la Mzambarauni Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam

John Philipo Kessy mfanyabiashara kutoka soko la Mzambarauni Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam

Kushoto ni mwandishi na msimamizi wa www.dkmadai.com, Kenneth Maganga akifanya mahojiano na Baraka Rashid kuhusu umuhimu wa matunda kiafya.

Hizo ni baadhi ya faida za matunda, lakini zaidi unaweza kuendelea kufuatilia tovuti hii ya www.dkmandai.com na tutaendelea kukuletea mfululizo wa makala na maelezo mbalimbali kuhusu matunda na umuhimu wake katika afya zetu, lakini pia tunakusihi endapo utakuwa unamatatizo yoyote ya kiafya na ungehitaji tiba nzuri na ya uhakika basi unaweza kufika Mandai Herbalist Clinic, Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na ukutane n Dk Abdallah Mandai na hakika utapona kabisa.

No comments:

Post a Comment