Sunday, 22 February 2015

JE, UMEISIKIA HII YA KIPIMO KIPYA CHA KUCHUNGUZA EBOLA?
Shirika la afya duniani (WHO) limeridhia kipimo kipya cha kuchunguza kirusi cha Ebola kwa binadamu.

Kipimo hicho kinaelezwa kuwa na uwezo wa kutoa majibu ndani ya dakika 15.

Hatua hiyo imeelezwa kuleta matumaini mapya katika harakati za kukabiliana na ugonjwa huo hatari ambao hadi sasa umeshaua watu zaidi ya 9200 wengi wao huko Liberia, Guinea na Sierra Leone.

WHO imeuelezea ugunduzi wa nyenzo hiyo mpya ni wa kihistoria kwani inaweza kutumika hata maeneo yasiyo na umeme na matumizi yake hayahitaji mafunzo ya kiwango cha juu.

Hata hivyo, WHO imesema matokeo ya kipimo hicho kilichotengenezwa na kampuni ya Kimarekani, bado si sahihi sana na yanapaswa kuthibitishwa na kipimo kingine kinachochukua muda mrefu, PCR.

Wakati hayo yakiendelea nako nchini Liberia wameamua kufungua mipaka ya nchi hiyo kufuatia kupungua kwa ugonjwa huo, ambapo rais wa nchi hiyo Ellen Johnson Sirleaf, alisema hatua zitachukuliwa kuhakikisha kuwa virusi vya Ebola havitoingia tena nchini humo kwa kupitia mpakani.

Nchi hiyo pia imesema itaondosha amri ya kutoka nje usiku

Endapo unasumbuliwa na magonjwa sugu basi wasiliana na Mandai Herbal Clinic kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. 

No comments:

Post a Comment