Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 23 February 2015

JE, UNATATIZO LA KUJIHISI MCHOVU KILA SIKU, ZIFAHAMU HAPA SABABU ZA TATIZO HILO NA UEPUKANE NAZOKuna baadhi ya  watu kila siku wamekuwa wakilalamika kuwa na uchovu na kuzongwa na hali ya uvivu muda wote, jambo ambalo hupelekea hata kushindwa kufanya shughuli zao nyingine za muhimu katika maisha.


Kuna sababu mbalimbali ambazo huweza kusababisha tatizo hili la kujihisi mchovu kila siku au mara kwa mara na miongoni mwa sababu hizo ni pamoja na kukosa usingizi.

Unapokosa muda wa kutosha wa kulala, basi tegemea kuwa mtu mwenye kuzongwa na hali ya uchovu kila siku, hii ni kwa sababu unapolala mwili nao unapata nafasi nzuri ya kupumzika hivyo mara unapoamka mwili unakuwa umeshapumzika kiasi cha kutosha hivyo inakuwa ni vigumu kupatwa na hali ya uchovu.

Kutokufanya mazoezi ni sababu nyingine inayoweza kupelekea mtu kujihisi mchovu kila siku, hivyo ni vizuri kuzingatia kufanya mazoezi kila siku angalau kwa dakika 30 tu pindi unapoamka na hii itakufanya kujisikia vizuri na kuondokana na hali ya uchovu.

Unywaji wa maji, watu wengi kunywa maji kwao huwa ni tatizo na hasa wanawake ndio mara nyingi wamekuwa wazito kidogo katika suala hili la kunywa maji, lakini maji ni muhimu sana katika miili yetu na yananafasi kubwa katika kuondoa tatizo hili la kuhisi uchovu kila mara, hivyo ni vizuri ukajenga utamaduni wa kunywa maji ya kutosha kadri uwezavyo.

Sababu nyingine ni kufanya kazi kwa muda mrefu tena bila kupata muda wa kupumzika, ni wazi kuwa kwa sasa kila mtu anapambana  kutafuta maisha ili aweze kujikimu yeye pamoja na familia, hivyo baadhi yao hujikuta katika kutafuta huko wanakosa hata muda wa kupumzika mara baada ya kazi, hivyo mtu kama huyu ni lazima atakuwa akisumbuliwa na shida hii ya kujihisi mchovu kila wakati, lwahiyo ni vizuri ukapata muda wa kupumzika kidogo mara baada ya kazi.

Hofu ni jambo jingine linaloweza kukuletea kuhisi uchofu wa mwili wako mara kwa mara, huenda hofu hiyo ikawa ni kuhusu kufukuzwa kazi na bosi wako, au kama wewe nidereva labda kila unapokuwa barabarani umekuwa ukihisi kusababisha ajali. 

Endapo unasumbuliwa na tatizo hili la hofu unaweza kulimaliza kwa kujihusisha na mazoezi au kuwashirikisha marafi au ndugu juu ya kile ambacho umekuwa ukikihofia kwa kufanya hivyo utaweza kumaliza tatizo hili la hofu sambamba na lile la kuwa mchovu.

Kutokunywa chai au kutoapata kifungua  kinywa asubuhi ni sababu nyingine ya mwili kuwa mchovu,hii ni kwa sababu unapopata kifungua kinywa asubuhi ni kama kuufanya mwili kuamka na nguvu mpya na hivyo husaidia kukuondosha na uchovu.
Sababu za hali hii ni nyingi kwa kweli isipokuwa hizo ni chache kati ya zile nyingi, lakini endapo utazingatia hayo basi kwa kiasi kikubwa itakusaidia kuepuka hali ya uchovu na uvivu kila siku.

Endapo unasumbuliwa na magonjwa sugu basi wasiliana na Mandai Herbal Clinic kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.  

No comments:

Post a Comment