Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 3 February 2015

JE UNAZIJUA SABABU ZA UKOSEFU WA HAMU YA KUSHIRIKI TENDO LA NDOA KWA WANAUME? DK MANDAI HAPA ANAFAFANUA
Mara nyingi ni nadra sana kusikia mwanaume anatatizo la  kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa, lakini ni wazi kwamba kuna baadhi ya wanaume hukabiliwa na tatizo hili nakujikuta wakikosa msisimko na hamu ya kufanya tendo hilo.


Mtaalam wa tiba asili kutoka Mandai Herbalist Clinic Dk Abdallah Mandai anasema kuwa tatizo hili huchangia msongo wa mawazo kwa wanaume wengi wanaosumbuliwa nalo pamoja na kusababisha mwanaume kuanza kupunguza ukaribu wa kukaa  na mwenzi wake kwa kuogopa pengine mpenzi wake atagundua kuwa anatatizo hilo. Hivyo wanaume wengi wenye tatizo hili hulazimika kutumia sababu nyingi za uongo kwa wapenzi wao kwa lengo la kupunguza ukaribu nao.

Dk Mandai anasema moja ya sababu za tatizo hili ni pamoja na suala la umri, hii ni kwa sababu mwanaume anavyozidi kuongezeka umri, ndivyo pia hupunguza shahuku na hamu ya kushiriki tendo la ndoa.

Mtaalam huyo anaendelea kusema kuwa, sababu nyingine ni matatizo ya msongo wa mawazo (stress), msongo huo wa mawazo unaweza kuwa unatokana na migogoro ya kifamilia, hali ngumu ya kiuchumi, mahusiano au magonjwa yananyoathiri mfumo wa fahamu (mental disorder)  nayo huweza kuwa chanzo cha tatizo hili.

Pia mtaalam huyo anabainisha kuwa, matatizo ya kiafya (deseases), ikiwa ni pamoja na baadhi ya magonjwa nayo huweza kumsababishia mwanaume kukosa hamu ya tendo la ndoa. Mfano wa magonjwa hayo ni pamoja na kisukari, presha ya kupanda, mafuta menge mwilini, UKIMWI n.k

Dk Mandai anasema sababu nyingine ni matumizi ya baadhi ya madawa, ambayo huweza kuwa chanzo cha tatizo hilo na hasa madawa yanayotumika  kwa wagonjwa wenye magonjwa yasiyoambukiza.

Mambo mengine yanayoweza kuwa chanzo cha tatizo hili ni mhusika kuwa na uchovu wa mara kwa mara, ulevi wa pombe kupita kiasi, uvutaji wa sigara na matumizi ya dawa za kulevya kama kokeini, heroin vyote hivyo huweza kuchangia tatizo hilo.

Mbali na sababu hizo, pia unene kupita kiasi huchangia tatizo hili kwani kadri unene unavyoongezeka hivyo hivyo huathiri uzalishaji wa ‘testo sterone hormone’ ambayo husaidia kuleta hamu ya kushiriki tendo la ndoa.

Hata hivyo, Dk Mandai anasema kuwa mwanaume mwenye tatizo hilo huweza kukabiliwa na tatizo la kushindwa kabisa kumridhisha mwanamke na hatimaye kuvunjika kwa mahusiano au ndoa, pia hushindwa kusimamisha sehemu zake za kiume, pamoja na kusongwa na mawazo ambayo pia huweza kupelekea matatizo mengine kama vidonda vya tumbo na presha ya kupanda.

Pamoja na hayo yote, Dk Mandai anasema tatizo hili huweza kutibika kwa kutegemea chanzo cha tatizo, lakini matumizi ya baadhi ya vyakula na matunda huweza kuwa ni msaada mkubwa wa kutatua shida hii. Mfano wa vyakula hivyo ni pamoja na zabibu, tikiti maji, tangawizi, parachichi, zabibu, tangawizi, pilipili,pweza, hivyo ni baadhi ya vyakula vinavyoweza kusaidia kuondokana na tatizo hili.

Sambamba na hayo, Dk Mandai anasema ni vyema ukawahi mapema kuonana na wataalam mara tu unapohisi kuwa na tatizo hili, hii itakusaidia kupata utatuzi wa kina juu ya tatizo hili, lakini pia unaweza fika Mandai Herbalist Clinic iliyopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa uchunguzi zaidi.

No comments:

Post a Comment