Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 13 February 2015

JUISI YA KOMAMANGA MSAADA KWA WANAWAKE
Kwa kawaida kipindi cha hedhi ni kati ya siku nne hadi saba, ambapo siku mbili za kwanza damu hutoka kwa wingi na baadaye hupungua na hatimaye kuacha.


Lakini iwapo katika siku zote za hedhi damu itatoka kwa wingi na ikaendelea kutoka kwa siku zaidi bila kuonesha hali ya kuacha, basi lazima kuwe na tatizo linalohitajika kupatiwa ufumbuzi.

Wakati mwingine hedhi inaweza kuja mapema sana au katika muda uliotarajiwa na hali hiyo pia huashiria kuna tatizo ambalo huhitajika kuchunguzwa zaidi.

Hata hivyo Dk Abdallah Mandai kutoka Mandai Herbalist Clinic anasema kuwa mtu mwenye tatizo hili anaweza kutengeneza glasi moja ya juisi ya komamanga na kuitumia wakati wa kifungua kinywa.

Anza tiba hiyo siku tatu kabla ya muda wa hedhi endapo tatizo hilo lilishatokea siku za nyuma au anza tiba utakapogundua kwamba tatizo limeanza, lakini tiba hiyo endelea nayo kwa siku mbili zaidi baada ya damu kuacha kutoka.

No comments:

Post a Comment