Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 16 February 2015

KAA TAYARI KWA HIKI KINGINE KUTOKA MANDAI ENTERTAINMENTTukiwa tunaendelea kukuelimisha kuhusu masuala ya tiba asilia na mambo ya afya kwa ujumla, tumeona ni vyema twende sambamba na Watanzania wote yaani kwa kuhakikisha wasomaji wetu wanapata elimu kuhusu masuala ya tiba asili (afya)  na sasa pia tutaanza kuwapa fursa wale wapenda habari za burudani nao kuanza kupata habari mbalimbali za burudani kupitia sisi.

Habari hizo zitakuwa zikiwahusu mastaa mbalimbali wa hapa ndani ya nchi na nje iwe ni kuhusu filamu, mziki, vichekesho na hata siasa na mengine mengi yatakayokuwa yakihusu jamii kwa ujumla, lakini burudani hizo zote utaanza kuzipata hivi karibuni kupitia www.mandaientertainment.com.

Huu ndio muonekano wa awali wa tovuti (website) yetu ya burudani itakavyokuwa ikionekana, kwa sasa bado inafanyiwa marekebisho ikiwa tayari tutakupa taarifa wewe mpenzi wa habari za burudani


Tunachoweza kusema ni kwamba kuanza kwa tovuti hii ya habari za burudani basi sio kwamba tovuti ya afya ya kuhusu tiba asili itakuwa haifanyi kazi, hapana bali tovuti yetu hii www.dkmandai.com ya kuhusu afya itaendelea kukuletea mimea tiba kila siku na namna inavyotibu magonjwa mbalimbali, hivyo usiache kuendelea kuitembea ili kujua mengi kuhusu mimea tiba na jinsi inavyofanya kazi nzuri katika miili yetu,

Isipokuwa pale utakapokuwa ukihitaji  kupata habari za burudani basi utakuwa ukiingia www.mandaientertainment.com na utakutana na masuala ya burudani yote huko.

Ukweli ni kwamba tunapenda kukuhudumia katika nyanja zote za kihabari msomaji wetu, hivyo endelea kutuunga mkono na kama unamatangazo au tukio lolote unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba, 0758 163 818, 0672 060 006. Au Barua pepe mandaitz@gmail.com. Karibu  gharama zetu ni za chini sana haijawahikutokea.

No comments:

Post a Comment