Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 10 February 2015

KAMA UNASHIDA YA MIGUU KUWAKA MOTO BASI HII INAKUHUSU SANA NI VIZURI UKASOMA

Matatizo ya aina hii mara nyingi huwapata watu ambao shughuli zao huwalazimisha kutembea kwa muda mrefu, kusimama kwa muda mrefu au kukaa kwa muda mrefu wakati miguu ikiwa imening’inia.

Dk Abdallah Mandai kutoka Mandai Herbalist Clinic anasema  kuwaka moto kwa miguu na nyayo husababishwa na mzunguko dhaifu wa damu katika miguu au ukosefu wa virutubisho na madini yanayohitajika mwilini.
 
Mtaalam huyo anabainisha kwamba, chakula cha asili kinahitajika zaidi ili kuondoa sumu zinazoleta athari hizi ndani ya mwili. Pamoja na kufanya mabadiliko katika aina ya vyakula vitakavyoliwa kwa ajili ya kupata virutubisho na madini muhimu.

Dk Mandai anaeleza baadhi ya tiba ambazo zinaweza kuondoa tatizo hilo kama ifuatavyo.

Limao
kuhusu limao mtaalam huyo anasema mhusika anapaswa kuosha miguu na nyayo kwa maji ya moto na sabuni na baadaye kukata limao katika vipande viwili kisha kupaka sehemu zile ambazo huwa unahisi kama kuungua. 

Maji ya uvuguvugu /chumvi.
Wakati umekaa, tumbukiza miguu ndani ya maji ya uvuguvugu, yaliyoongezewa na chumvi ya mawe yakiwa ndani ya karai kwa muda wa nusu saa, lakini wakati umetumbukiza miguu unakuwa unaosha sehemu ambazo huwa unajihisi kuwaka moto.

Msubili
Osha miguu na nyayo kwa maji moto na sabuni, kisha pondaponda jani la msubili na upake sehemu zote unazojihisi kuungua.

Hizo ni baadhi tu ya tiba ya tatizo hilo, lakini kwa maelezo zaidi kuhusu tiba hii unaweza kufika Mandai Herbalist Clinic iliyopo Mongolandege jijini Dar es Salaam na utakutana na wataalam wetu na kupata maelekezo zaidi.

No comments:

Post a Comment