Advertisement

Advertisement

Shop

Shop

Mixer

Mixer

Tuesday, 17 February 2015

KAMA UNASUMBULIWA NA MAFUA UNAWEZA KUTUMIA LIMAO KAMA TIBA
Mafua ni ugonjwa ambao chanzo chake ni kuathirika kwa mirija ya kichwani ya mfumowa kuvuta pumzi. Athari hizo huletwa na virusi vya aina mbalimbali kupitia kwenye hewa au mavumbi na ni ugonjwa unaoambukizwa kwa haraka sana.


Miongoni mwa dalili za mafua ni pamoja na kuumwa kichwa na homa kidogo, kikohozi au kukereketwa kohoni, kuchuruzika kwa kamasi (aina ya majimaji) puani pamoja na uchovu na maumivu ya maungo.

Aidha, njia pekee ya kujikinga na mafua ni kujenga kinga ya mwili kwa kufuata kanuni za afya bora, lakini dawa zote zinazotumika kwa ajili ya kutibu mafua ni kujaribu kumwezesha mgonjwa arudi hali ya kawaida mapema iwezekanavyo.

Moja ya tiba ninayopenda kukujuza leo kutoka kwetu Mandai Herbalist Clinic ni hii ya kutumia limao, ambapo umhusika anapaswa kutengeneza juisi ya limao moja katika glasi ya maji ya uvuguvugu.Ongeza kijiko kimoja cha mezani cha asili kisha koroga vizuri na kunywa polepole  na uatatkiwa kutumia tiba hii asubuhi na jioni kwa muda wa siku tatu.  

Mbali na tiba hiyo ya limao pia bamia, ukwaju, pilipili manga, tangawizi navyo pia ni miongoni mwa tiba nyinginezo za mafua.

Unaweza kufika Mandai Herbalist Clinic endapo unasumbuliwa na magonjwa yoyote na hakika utapata tiba nzuri na sahihi na kupona kabisa shida inayokusumbua. Kliniki ipo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.Au piga simu namba, 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com 

1 comment:

  1. Mimi nimetumia dawa nyingi zikiwemo hizo ambazo ni tangawizi....limao na kadharika lakini mbona bado mafua hayaishi tena yamekuwa yakinisumbua sana wakati wa asubuhi napo amka na nnapokuwa mwenye joto

    ReplyDelete