Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 21 February 2015

KAMA WEWE NI MNENE KUPITA KIASI NA UNAPENDA KUPUNGUA, HEBU JARIBU NJIA HIZI CHACHE


Unene ni moja ya sababu inayochangia kusababisha baadhi ya magonjwa, hivyo ni vizuri kuepuka unene kupita kiasi endapo unaweza kufanya hivyo.
Katika kuhakikisha unaepukana na unene inakupasa kufanya mazoezi, ambayo yatakusaidia kupunguza uzito hususani katika kipindi cha miezi sita ya awali na kuufanya mwili kuwa na uzito wa kawaida.

Pia kabla ya kuanza mazoezi inashauriwa kuonana na wataalam ili kupata ushauri juu ya mazoezi yapi yatakayokufaa kupunguza mwili wako katika hali nzuri.

Jambo jingine ambalo ni muhimu katika kupunguza unene ni kukubali kubadili tabia, ikiwemo kuhusu namna unavyokula, ambapo mtu mnene unapaswa kupunguza kiwango cha chakula unachokula na badala yake ule chakula kiasi lakini chenye kusheheni virutubisho vya kutosha ambavyo vitaufanya mwili wako kuendelea kubaki na afya nzuri.

Mbali na njia hiyo, pia massage huweza kusaidia kupunguza unene, kwani inaelezwa kuwa unapofanyiwa massage angalau mara moja au mbili kwa mwezi basi husaidia mwili kuwa katika hali nzuri, hii ni kutokana na zoezi hilo kuhusisha mwili kwa ujumla.

Unaweza kuanza kutangaza na tovuti yetu hii kwa gharama nafuu sana msomaji wetu, wasiliana nasi kwa simu namba, 0758 163 818, 0672 060 006 . Karibu.

No comments:

Post a Comment