Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 20 February 2015

KAMA WEWE NI MZAZI NA UNASHIDA YA KUTOA MAZIWA MACHACHE BASI TUMIA MBINU HII
Kuna baadhi ya wanawake wanapojifungua (kuzaa) hujikuta katika changamoto ya kupata maziwa hafifu kwa ajili ya mtoto na hivyo kupelekea mtoto kushindwa kushiba vizuri anapokuwa akinywa maziwa hayo.


Hata hivyo, kuna njia kadhaa zinazoweza kutumika katika kurekebisha hali ya utoaji wa maziwa ya mama moja ya njia hizo ni hii ya kutumia ufuta.

Mtaalam wa tiba asilia kutoka Mandai Herbalist Clinic anasema kuwa, unachotakiwa kufanya ni kuchukuwa kijiko kimoja cha chai cha ufuta kisha weka ndani ya lita moja ya maji.

Baada ya hapo chemsha kwa muda wa dakika 20 na kisha acha maji yapoe (vuguvugu) chuja na uumpe mzazi anywe yote na kula ufuta kwa ajili ya kuongeza utoaji wa maziwa.

Hiyo ni njia mojawapo inayoweza kumsaidia mzazi katika kuongeza kiwango cha utokaji wa maziwa kwa mama , lakini kama ungependa kuzifahamu njia nyingi zaidi endelea kufuatilia tovuti hii kila iitwapo leo. Au fika kliniki kwetu Mandai Herbalist Clinic iliyopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.Simu namba  0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment