Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 28 February 2015

KAPTENI JOHN KOMBA AFARIKI DUNIA
Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mwimbaji maaarufu wa nyimbo za Siasa nchini Tanzania, Keptain John Komba amefariki dunia Jumamosi hii jioni.


Kwa mujibu wa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye alisema kifo cha mbunge huyo kimetokea siku ya Jumamosi majira ya jioni.

Marehemu Kaptain Komba alizaliwa tarehe 18 mwezi March mwaka 1945 na alipata elimu ya msingi katika Shule ya Lituhi kisha kupata elimu ya sekondari katika shule ya Sekondari ya Songea kuanzia mwaka 1971 hadi mwaka 1974.

Mwaka 1975 hadi mwaka 1976 Marehemu John Komba alijiunga na chuo cha ualimu kilichopo Kleruu Iringa, ambapo alihitimu ngazi ya cheti cha ualimu.

Marehemu John Komba pia ni mwanajeshi ambaye alipata mafunzo ya uafisa wa Jeshi katika Chuo cha Maafisa wa Jeshi kilichopo Monduli mwaka 1978 hadi mwaka 1978.

Keptain John Komba pia alipata mafunzo mengine ya siasa kutoka Chuo Kikuu cha Washngton International ambapo alitunukiwa shahada ya siasa mwaka 2006 hadi mwaka 2008.

Mandai Herbal Clinic tunapenda kutoa pole kwa ndugu wa karibu na jamaa pamoja na Watanzania wote kwa ujumla kwa kuondokewa na ndugu yetu Kapteni John Komba. R.I.P Kapteni John Komba

No comments:

Post a Comment