Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 3 February 2015

KARANGA NI KINGA YA MAGONJWA YA MOYO
Watu wengi tunakula karanga pasipo kufahamu umuhimu wake katika afya zetu, kwani miongoni mwetu hudhani karanga ni kama kiburudisho tu, lakini ukweli ni kwamba karanga si chakula cha kupuuzwa kutokana na faida zake.

Dk Abdallah Mandai ni mtaalam wa tiba asili hapa nchini kupitia kliniki yake iitwayo Mandai Herbalist Clinic yeye anasema karanga ni moja ya dawa nzuri na tena ni mlinzi wa magonjwa ya moyo maana haina ‘cholesterol’ ( lehemu).

Mtaalam huyo anaendelea kusema kwamba, ukila pamoja na ile sukari guru ya mgando (jiggery) inajenga kinga na ulinzi dhidi ya mashambulizi ya maradhi ya ini na kifua kikuu.

Aidha, karanga ni chanzo kizuri cha protini, lakini pia husaidia sana kulinda aina fulani ya saratani na inakiwango cha juu cha ‘calcium’,copper’ na ‘phosphorus’ na ‘sodium.

Pamoja na hayo, Dk Mandai anaeleza kuwa karanga pia ni nzuri kwa kisukari, na mhusika anapawa kula wastani wa kiganja cha mkono kwa siku.

Karanga pia inaelezwa kusaidia kuepukana na kiharusi (stroke) ambapo kwa mujibu wa utafiti uliofanywa maabara na kuchapishwa kwenye Jarida la Kilimo na Kemia ya Chakula (Journal of Agricultural Food Chemistry), umeonesha kuwa kirutubisho aina ya ‘resveratrol’ ambacho kinaelezwa kupatikana katika karanga husaidia kirutubisho hicho huimarisha utembeaji wa damu kwenye mishipa inayokwenda kwenye ubongo kwa kiasi cha asilimia 30.

Mbali na hayo Dk Mandai atoa tahadhari kwa wale wanaougua jongo (gout) au wenye matumbo dhaifu wanapaswa kuepuka kula karanga kwa sababu zinapokaangwa hutoa ‘uric’ ambayo huathiri mwili.

Ikiwa unasumbuliwa na magonjwa sugu unaweza kufika kliniki ya Mandai Herbalist Clinic kituo kilichopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na utapata ufumbuzi wa magonjwa hayo.

No comments:

Post a Comment