Friday, 13 February 2015

KITUNGUU SWAUMU KINASAIDIA KUONDOA MAUMIVI YA KIUNOBila shaka umewahi kusikia mtu akikwambia kuwa anasumbuliwa na maumivu ya kiuno, kwani hili ni moja ya tatizo ambalo huwakuta baadhi ya watu kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za mfumo wa maisha pamoja na shughuli tunazozifanya kila siku.


Miongoni mwa sababu zinazoweza kuchangia maumivu ya kiuno ni pamoja na uzito mkubwa wa mwili, kukaa isivyostahili kwa muda mrefu, kusimama muda mrefu au kubeba mizigo mizito.

Sababu nyingine ni kutokuwa na mazoezi, kula chakula kisichofaa, kukosa choo (constipation) matatizo katika mfumo wa uyeyushaji wa chakula  pamoja na matatizo wakati wa kipindi cha hedhi kwa wanawake.

Baadhi ya tiba zinazoweza kukusaidia kukabiliana na tatizo hili ni pamoja na matumizi ya kitunguu swaumu, ambapo mhusika atatakiwa kutafuna punje sita za kitunguu swaumu kila siku na kupondaponda punje moja ya kitunguu swaumu kisha kupaka sehemu ya kiuno inayouma akabla ya kwenda kulala.
 
Kitunguu swaumu
Mbali na kitunguu swaumu pia mchaichai, msubili na mafuta ya mkaratusi husaidia sana kumaliza shida hii ya maumivu ya kiuno endapo vyote hivyo vitatumika ipasavyo.

Unaweza kufika kliniki yetu ya Mandai Herbalist Clinic iliyopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na utapata tiba ya magonjwa mbalimbali yanayokusumbua. Au piga simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443

No comments:

Post a Comment