Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 20 February 2015

KOMAMANGA NI DAWA YA UGONJWA WA FIZI ZA MENO
Ugonjwa wa fizi za meno ni ugonjwa ambao huathili ngozi nyembamba inayozunguka mizizi  ya meno na kusababisha utungaji wa usaa, kulegea kwa meno na kusinyaa kwa fizi.


Ugonjwa  huu ukiendelea,unaweza kusababisha matatizo katika uyeyushaji wa chakula kwa sababu ya mlundikano wa uchafu tumboni, unaotoka kwenye fizi za meno.

Hata hivyo, mtaalamu wa tiba asili, Dk Abdallah Mandai kutoka  Mandai Herbalist Clinic anasema kuwa komamanga ni moja ya tiba nzuri kwa ugonjwa wa fizi za meno. 

Dk Mandai anasema unatakiwa kuchukua kijiko kimoja cha chai cha unga wa ganda la tunda la komamanga, kisha ya ongeza nusu kijiko cha chai cha pilpili manga na chumvi nusu kijiko.

Baada ya hatua hizo changanya vizuri kwa pamoja katika nusu lita ya maji kisha tumia maji hayo kwa kusukutua mara tatu kwa siku endeleza tiba hiyo kwa siku kumi na nne.

Endapo unasumbuliwa na magonjwa sugu basi wasiliana na Mandai Herbalist Clinic kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment