Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 28 February 2015

KULALA SANA HUSABABISHA KUPATA UGONJWA WA KIHARUSI
Imeelezwa kuwa watu wanaolala kwa zaidi ya masaa nane kwa siku wapo katika hatari ya kupata ugonjwa wa kiharusi.


Hayo yamebainika kufuatia utafiti uliohusisha takribani watu 10,000 katika Chuo Kikuu cha Cambridge, ambapo ulibaini kuwa wale wanaolala kwa takribani saa nane wana uwezekano mkubwa wa asilimia 46 kupata kiharusi.

Aidha, watu wazima ndio hupendelea kulala kati ya saa sita na tisa ili kupumzika vizuri, lakini kulala zaidi hushirikishwa na matatizo ya afya kama vile ugonjwa wa sukari pamoja na ule wa kunenepa kupita kiasi.

Hata hivyo pamoja na utafiti huo, lakini haikubainika iwapo kulala kwa zaidi ya saa nane huenda ndiko kunakosababisha matatizo hayo ambayo husababisha kiharusi au iwapo ni miongoni mwa sababu za magonjwa yasiojulikana.

Kitengo cha ugonjwa wa kiharusi
Taarifa zinasema kwamba utafiti huo ulifanywa miongoni mwa watu wenye umri kati ya miaka 42 na 81 ambapo watafiti walichunguza mienendo yao ya kulala kwa kipindi cha miaka 10 ambapo watu 346 walipatwa na kiharusi.

Baada ya kuangazia athari kama vile miaka na jinsia, watu waliosema wamekuwa wakilala kwa zaidi ya masaa nane walipatikana na hatari ya asilimia 46 kupatwa na ugonjwa huo, huku wale walioweza kulala kwa chini ya masaa sita walipatikana na hatari ya asilimia 18.

Sambamba na hayo yote utafiti umesema lakini wataalam hawajua sababu yake.
BBC NEWS

No comments:

Post a Comment