Wednesday, 11 February 2015

MAJANI YA MPERA YANAPOCHEMSHWA HUSAIDIA KUZUIA KUTAPIKA

Mara zote unapokula kitu muhimu ni kuhakikisha unafurahia mlo wako, lakini inapotokea chakula au mlo wako unakuwa ni moja ya sababu ya kukufanya kupatwa na kichefuchefu na hatimaye kutapika basi jua huenda kuna tatizo katika mfumo wa uyeyushaji chakula (digestive  system)


Kichefuchefu na kutapika mara nyingi huwa na uhusiano na mfumo wa uyeyushaji wa chakula ndani ya tumbo na iwapo kutapika huko kumechangiwa na mzio (allergy) wa chakula, kula kupita kiasi au sumu ndani ya chakula ni vyema ukaendelea kutapika kuliko kuizuia hali hiyo kuendelea ili chakula kilivhopo tumboni kitoke na baada ya kumaliza kutapika hali yako itarudi kama kawaida.

Lakini iwapo kuna haja au umuhimu wa kuzuia kutapika ili kukinga athari kubwa zinazoweza kujitokeza kutokana na kutapika huko mfano kupungukiwa kiwango cha maji mwilini basi ni vizuri ukatumia njia hii katika kuzuia kutapika.

Unaweza kutumia majani ya mpera kwa kuyachemsha vizuri kwa muda wa dakika 20 kisha mhusika anywe nusu glasi ya maji hayo ili kuzuia kutapika na rudia kunywa tena baada ya saa moja hadi kutapika kutakapopona.

Pia unaweza kufika Mandai Herbalist Clinic ili upate suluhsho la magonjwa mengine yakiwemo yale sugu kwa kutumia tiba asili za mimea na matunda, kituo chetu kipo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment