Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 2 February 2015

MAJI YANAUWEZO MKUBWA WA KUOKOA MAISHA YAKOKunywa maji safi na salama kwa kiasi kinachostahili kiafya kunaweza kuboresha maisha na kumfanya mtu ajihisi mwenye afya na furaha zaidi, hivyo kunywa maji ya kutosha kuna faida nyingi.
Hivi unajua kwamba, wakati unapotoka jasho kikombe kimoja cha maji hupungua mwilini mwako? Na je, unatambua kwamba iwapo utaoga wakati wa mchana kwa mara tatu kwa siku ni sawa umekunywa vikombe 6 vya maji?


Mtaalam wa tiba asili Dk Abdallah Mandai anabainisha kuwa kunywa maji kwa kiasi cha kutosha husaidia kupunguza uwezekano wa kutokea mawe katika figo na hulainisha viungo pamoja na kuzuia mafua.

Asilimia 60 ya uzito wa binadamu ni maji na mfumo wa mwili hutegemea maji ili kufanya kazi zake. Hivyo ukosefu wa maji mwilini humfanya mtu akaukiwe na maji au ‘dehydration,’ hali ambayo hutokea pale mtu asipokuwa na maji ya kutosha mwilini ya kuuwezesha mwili wake kufanya kazi zake za kawaida. 

Adha, mtaalam huyo anasema kuwa maji huboresha afya ya ngozi. Kunywa maji ya kutosha hupendezesha ngozi na kuipa muonekano mzuri na husaidia kuboresha tishu za ngozi na kuongeza unyevu kwenye ngozi.

Dk Mandai anaendelea kueleza kuwa, faida nyingine ya maji ni pamoja na kusaidia katika utendaji wa ubongo hii ni kwa sababu maji huuweka ubongo katika hali nzuri zaidi na ya ufanisi. Kwa mantiki hiyo basi kunywa maji ya kutosha kunamwezesha mtu kufikiria vyema zaidi.

Faida nyingine za maji ni kupunguza uwezekano wa kupata baadhi ya magonjwa, ikiwemo matatizo yam awe ya figo, matatizo ya ini pamoja na baadhi ya saratani vyote huweza kuzuiwa kwa kunywa maji.

Mtaalam  huyo anasema kuwa kwa wale wenye shida ya kupata haja kubwa constipation, wanapokunywa maji ya kutosha huweza kuwasaidia kuanza kupata chaja kubwa laini na kuepuka tatizo la kupata haja kubwa ngumu.

Pamoja na hayo, Dk Mandai anasema ni vizuri kunywa vikombe viwili vya maji asubuhi mara unapoamka, kwani husaidia kuamsha viungo vya ndani ya mwili, lakini pia ni vizuri kunywa kikombe kimoja cha maji dakika 30 kabla ya mlo, kwani husaidia kupata choo vizuri.Vilevile kunywa kikombe kimoja cha maji kabla ya kulala kwani kwa kufanya hivyo huzuia shinikizo la moyo.

Mbali na hayo, pia Dk Mandai hapa anamalizia kwa kukufahamisha dalili za ukosefu wa maji mwilini ambazo ni pamoja na kuhisi uchovu, kichwa kuuma, kuhisi kiu sana, mdomo kukauka, kukosa haja ndogo (mkojo), huku dalili nyinginezo zikiwa ni mhusika kuhisi kizunguzungu na udhaifu wa misuli.

Unaweza kufika Mandai Herbalist Clinic kwa huduma mnalimbali za kiafya, kituo kipo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment