Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 6 February 2015

MAMBO YA KUZINGATIA IKIWA UNASUMBULIWA NA VIDONDA VYA TUMBOTatizo la vidonda vya tumbo ni moja ya shida ambayo inawasumbua watu wengi kwa sasa, huku mhusika mara nyingi huwa anajikuta anapata tabu sana namna ya kukabiliana na maumivu makali. Lakini ni vizuri ikiwa unasumbuliwa na tatizo hili ukazingatia kuacha kutumia kahawa na chai, hii ni kwa sababu matumizi ya vinywaji hivyo huongeza kiwango cha asidi kinachotengenezwa tumboni na badala yake unaweza kutumia chai herbal tea kama mbadala.

Pia ni vizuri ukazingatia kula kidogo kidogo mara kwa mara, hii husaidia kupunguza aside inayotengenezwa tumboni.

Jitahidi kuepuka na kuacha kutumia, vinywaji ambavyo vianavileo (pombe) vinywaji hivyo huchangia kutonesha vidonda vya tumbo na kusababisha kushindwa kupona haraka.

Acha kutumia, matumizi ya viungo katika vyakula, kwani hivyo navyo huchangia kuongeza mhusika kuwa na hali mbaya zaidi.

Hali kadhalika, unapokuwa uanasumbuliwa na vidonda vya tumbo ni vizuri kama ulikuwa ni mtumiaji wa sigara ukaacha kabisa, kwani uvutaji wa sigara utakuweka katika hatari zaidi ya kuzua vidonda vipya na kuzuia vile vya awali navyo visipone.

Hata hivyo, kwa mujibu wa mtandao wa healthandcure.com uliwahi kuwanukuu baadhi ya wataalam wa afya wakieleza kwamba, watu wanaosumbuliwa na maradhi ya mfumo wa chakula kama vile vidonda vya tumbo wanaweza kupata ahuweni au kupona kabisa ikiwa watakula bamia.

Kama unasumbuliwa na tatizo hili la vidonda vya tumbo unaweza kufika Mandai Herbalist Clinic, kituo kilichopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na utafanyiwe uchunguzi zaidi pamoja na kupata dawa za tatizo hilo.

No comments:

Post a Comment