Saturday, 21 February 2015

MATATIZO YA KUFUNGA CHOO (CONSTIPATION) NA NAMNA LIMAO LINAVYOWEZA KUWA TIBAKwa kawaida tunapokula chakula kila siku, lengo huwa ni kuahakikisha mwili unapata nguvu ili kuendelea kuishi, lakini chakula chochote kinacholiwa lazima kitumike mwilini na mabaki yake kutolewa kwa njia ya haja kubwa.


Hata hivyo, baadhi ya watu huwa wanakabiliwa na tatizo la kukosa choo , ambapo tatizo hili pia huambatana na tatizo la kupata choo kigumu.

Kwa kawaida, mtu anapopata tatizo hili hutumia muda wake mwingi chooni akijaribu kusukuma haja kubwa wakati mwingine bila mafanikio. Huku ugumu wa kuitoa haja hiyo ukiwasababishia maumivu makali.

Kitaalam kukosa choo kwa siku moja,  siyo tatizo, isipokuwa iwapo mtu atakosa choo kwa angalau zaidi ya siku tatu basi huenda likawa ni tatizo.

Zipo sababu nyingi  zinazoweza kusababisha tatizo hili zikiwemo za kutojizoeza kwenda haja kubwa mara kwa mara, kula vyakula vilivyokobolewa,  matumizi mabaya ya dawa, mabadiliko ya homoni na magonjwa mengine ya mwili.

Sababu nyingine ni udhaifu wa misuri ya tumbo, kutokuwa na mazoezi ya kutosha, kula nyama kwa kiasi kikubwaa pamoja na kula vyakula visivyofaa kwa ujumla.

Dalili za tatizo hili ni kutoenda choo mara kwa mara, kutoa kinyesi ambacho ni kigumu sana, kujitokeza chunusi nyingi mara kwa mara na kukosa hamu  ya chakula nk.

Moja ya tiba inayosaidia katika kuondokana na shida hii ni pamoja na matumizi ya maganda ya limau.Ambapo mhusika atapaswa kumenya maganda kisha kuyakatakata katika vipande vidogo vidogo na uondoe mbugu zote ndani ya limao.

Baada ya hapo loweka maganda ya limao pamoja na mbrgu zake katika glasi moja ya maji ya moto kwa usiku mzima, asubuhi utakunywa maji baada ya kuyachuja na kabla ya chakula chochote.

Endapo unasumbuliwa na magonjwa sugu basi wasiliana na Mandai Herbalist Clinic kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment