Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 21 February 2015

MATATIZO YA UTI NA VYANZO VYAKEUTI ni tatizo kubwa ambalo linasumbua zaidi watoto, wanawake na hata wanaume ingawa si kwa asilimia kubwa.

UTI ni kirefu cha Urinary Track Infection ni tatizo linaloikabili sekta ya afya kwa sasa.


Mtindo wa mavazi pia ni kati ya sababu ambayo, husababisha watoto kupata ugonjwa huo pale ambapo mtoto huyo huachwa na haja ndogo ama kubwa kwa wakati mrefu.

Mkurugenzi wa kituo cha tiba mbadala cha Mandai Herbal Clinic, Dkt Abdallah Mandai anasema tatizo hili hujitokeza pale mlango wa njia ya haja ndogo unaposhambuliwa na bacteria aina ya Escherichia coli.

Aidha, mtaalam huyo anasema kuwa bacteria hao husambaa na wasipotibiwa mapema huenea kwenye figo na athari zake huweza kuwa mbaya zaidi.

Bakteria hao hupatikana ndani ya sehemu za siri za mwanamke, lakini bacteria hao wanapokuwa ndani ya uke huwa hawana madhara, lakini mara inapotokea michubuko bacteria hao huanza kuathiri kibofu  cha mkojo na mtu huanza kupata madhara.

Dkt Mandai anaeleza kuwa wanawake hupata hupata UTI kwa urahisi sana kwa sababu mirija ya mkojo ya mwanamke ni mifupi hivyo huruhusu bacteria kupenya kwa urahisi tofauti na wanaume.

Sababu ambazo huweza kuchangia kupata ugonjwa huu ni pamoja na mtindo wa kujamiana kinyume na maumbile, hii ni sababu ya mwanamke kuweza kupata ugonjwa huu wakati wa kujisafisha.

Anafafanua kuwa, kutokana na hali halisi ya maumbile ya sehemu ya haja kubwa mtu anayetumika kinyume cha maumbile anaweza kupata UTI. 

Daktari anabainisha kuwa wakati wa ngono msuguano huwa mkubwa ambao hufanya bacteria kutoka kupitia majimaji na kuweza kuingia ukeni katika njia ya mkojo pale wakati mwanamke anapokuwa akijisafisha bila kuchukua tahadhari.

Pia mwanamke ambaye hufanya ngono mara kwa mara huwa katika hatari zaidi ya kupata ugonjwa huu kuliko Yule ambaye hufanya tendo hilo mara chache.

Sababu nyingine ni matumizi ya maji machafu wakati wa kujisafisha au kuoga, ambayo huweza kuweka bacteria kwa urahisi na mwanamke kupata UTI.

Hali kadhalika matumizi ya vyoo visivyo safi huweza kusababisha mtu kupata ugonjwa huu, hii ni kutokana ndani ya choo huwa na bacteria wengi wanaoweza kusababisha ugonjwa huu.

Mbali na hayo Dkt Mandai anasema kuwa kubana mkojo kwa muda mrefu nayo ni sababu ya kupata ugonjwa huu wa UTI.

Pamoja na hayo, Dkt Mandai anasema kuwa ugonjwa wa UTI huweza kutibika vizuri iwapo mtu atafika Mandai Herbal Clinic iliyopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam, huku akiwasihi Watanzania kuacha kutumia dawa hovyo bila kupata ushauri kutoka kwa wataalam wa afya.


Endapo unasumbuliwa na magonjwa sugu basi wasiliana na Mandai Herbalist Clinic kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. 

No comments:

Post a Comment