Advertisement

Advertisement

Shop

Shop

Mixer

Mixer

Thursday, 12 February 2015

MATUMIZI YA ZABIBU NA MCHICHA HUSAIDIA KUKABILIANA NA TATIZO LA UPUNGUFU WA DAMU MWILINI
Kunapokuwa na upungufu wa chembechembe nyekundu (hemoglobin) ndani ya damu basi mtu huyo anasemekana kuwa na upungufu wa damu.


Upungufu wa damu hutokea iwapo mafuta (marrow) ndani ya mifupa hayatatengeneza chembechembe nyekundu za damu za kutosha, au upungufu wa chakula chenye madini ya chuma, kutopata vitamin na protein ya kutosha aumhusika kuvuja damu nyingi.

Miongoni mwa vyakula vinavyoweza kukuongezea damu ni pamoja na mchicha, ambapo unatakiwa kutumia juisi ya mchicha nusu glasi kila baada ya mlo wa asubuhi, mchana na jioni, kisha baada ya wiki mbili unaweza kwenda hospitali kupimwa kiwango cha damu. 

Tunda za Zabibu

Zabibu pia ni moja ya matunda yenye uwezo mkubwa wa kuongeza damu mwilini, ambapo mhusika wa tatizo hili anashauriwa kutumia zabibu zilizokaushwa kwa muda wa wiki tatu.

Hali kadhalika pia matumizi ya soya ni msaada mkubwa katika kuongeza damu mwilini, ambapo itatakiwa kutumika katika chai au uji na mara nyingine hata kwenye ugali kwa kiasi cha muda wa wiki tatu.

Msomaji wetu hivyo ni baadhi ya vyakula ambavyo vinaweza kuwa msaada kwako ikiwa unatatizo la upungufu wa damu mwilini, hivyo hakikisha unazingatia matumizi yake na kwa hakika utajionea matokeo mazuri.

Unaweza kufika kliniki yetu iitwayo Mandai Herbalist Clinic iliyopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na utapata matibabu ya magonjwa yote sugu yanayokusumbua.

No comments:

Post a Comment