Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Sunday, 1 February 2015

MAZIWA MTINDI HULINDA AFYA ZETUMaziwa mgando (mtindi) yamekuwa yakitajwa kuwa ni miongoni mwa vyakula bora kutokana na kuwa na virutubisho vingi vya aina mbalimbali ambavyo vina faida nyingi katika mwili wa mwanadamu.

Miongoni mwa virutubisho vinavyopatikana katika maziwa ya mgando (mtindi) ni pamoja na 'calcium,' 'phosphorus,' 'riboflavin' (vitamin B12), 'potassium,' 'iodine' na vinginevyo.

Maandalizi ya kinywaji hiki hukamilika pale ambapo yanapokuwa yamesindikwa kwa kipindi cha mda Fulani, jamii nyingi zimekuwa zikifanya hivyo hapa nchini hususani jamii ya Wamasai na Kimang’ati, ambao huyaweka maziwa hayo kwenye kibuyu.

Mbali na kuwa virutubisho hivyo vinapatikana ndani ya maziwa ya mgando ambayo wengi tunayafahamu kama mtindi, pia hupatikana bakteria hai ambao ni muhimu kiafya katika mwili wa binadamu (probiotics).

Watafiti wamebaini kuwa bakteria wanaopatikana katika mtindi huweza kurefusha maisha kwa wazee, ni kinga kubwa kwa kina mama kutokana na maambukizo ya magonjwa ya ukeni na hata hupelekea kupunguza kiwango kikubwa cha shinikizo la damu la juu (high blood pressure level).

Wataalam hao kupitia tafiti hizo wamesema kuwa maziwa ya mgando (mtindi) yameokoa maisha ya walio wengi baada ya tathimini kutoka kwa wagonjwa zaidi ya 540 waliosumbuliwa na tatizo la shinikizo la damu.

Pamoja na hayo, idadi kubwa ya wagonjwa waliotumia kinywaji hiki walifanikiwa kupona baada ya muda usiopungua wiki nane, hivyo inapendekezwa kutumia kinywaji hiki kama sehemu ya lishe yetu.

Hata hivyo, inashauriwa kuhakikisha unatumia maziwa mtindi halisi yaliyotokana na maziwa ya ng'ombe na isiwe mtindi uliotengenezwa kwa maziwa ya ung.

Ikiwa unasumbuliwa na magonjwa sugu unaweza kufika kliniki ya Mandai Herbalist Clinic kituo kilichopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na utapata ufumbuzi wa magonjwa hayo.

No comments:

Post a Comment