Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Sunday, 1 February 2015

MAZOEZI NI MUHIMU NA HUSAIDIA KUEPUKANA NA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA


Mara nyingi tumekuwa tukipata ushauri kutoka kwa wataalam wa afya kuhusu umuhimu wa kufanya mazoezi kwa lengo la kulinda afya zetu na kuzifanya kuwa na uwezo zaidi katika kukabiliana na magonjwa mbalimbali.

Lakini leo tutaangalia umuhimu wa kufanya mazoezi hasa kwa watu wenye kusumbuliwa na kisukari, mara nyingi watu wenye kisukari huhamasishwa kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuweka kiwango cha sukari vizuri, lakini kubwa zaidi ni kujiondoa katika hatari ya kupata magonjwa ya moyo.

Mtaalam wa tiba asili Dk Abdallah Mandai anasema kuwa, mazoezi husaidia kuboresha kiwango cha sukari mwilini, hii ni kutokana na ukweli kuwa misuli inayofanya kazi hutumia sukari nyingi zaidi ya ile isiyofanya kazi.

Mtaalam huyo, anaeleza kwamba kuvutika kwa misuli hiyo kwa kiasi kikubwa huchangia kuzifanya seli za misuli kutumia sukari nyingi zaidi na kupunguza kiasi cha sukari kwenye damu. Faida nyingine ya mazoezi ni pamoja na kuboresha afya ya moyo, kudhibiti uzito wa mwili na msongo wa mawazo.

Dk Mandai anabainisha kwamba pamoja na kuimarisha mfumo wa moyo na misuli ya mwili, watu wengi hufanya mazoezi kwa ajili ya kujiweka sawa, kupunguza au kuimarisha uzito wa mwili kiafya, lakini pia husaidia kuongeza ujuzi wa umahiri katika michezo.

Anafafanua kuwa watu huhamasishwa kufanya mazoezi kwa ajili ya kuchochea kinga ya mwili na kuukinga mwili dhidi ya moyo, kupooza, kisukari aina ya pili, saratani pamoja na maradhi mengine.
Jambo la muhimu ni kwamba mazoezi humsaida mtu kumuondoa katika hatari ya kupata magonjwa sugu kwa asilimia 50, pia kukuondoa kwenye hatari ya kukupoteza maisha kwa asilimia 30.


Aidha, Dk Mandai anaendelea kueleza kwamba faida nyingine za mazoezi kwa afya ni pamoja na kusaidia kuboresha mifumo mbalimbali ya mwili, kuboresha afya ya akili, kuchochea kujiamini, kusaidia kupata usingizi wa kutosha pamoja na kuondoa hatari ya kupata magonjwa yanayotokana na msongo wa mawazo.

Mbali na hayo Dk Mandai anasema kuwa kitu kizuri ni kwamba,  mazoezi huwa hayagharimu kiasi chochote cha pesa na yanaweza kufanyika mahala popote, huku yakiwa na uwezo mkubwa wa kukupa matokeo ya haraka zaidi.


Sambamba na hayo, Dk Mandai anasema kuwa, inashauriwa kufanya mazoezi angalau mara moja kwa siku kwa kutumia dakika 30.

Kuna mazoezi mbalimbali yanayoweza kukufanya kuwa mwenye afya nzuri miongoni mwa hayo ni pamoja na kutembea kwa haraka, kukimbia, kuendesha baskeli, kucheza mpira, kufanya mazoezi ya viungo hata ukiwa chumbani kwako.

Mtanzania mwenzangu kumbuka kwamba mazoezi ni tiba na kinga ya magonjwa, hivyo anza sasa kupenda mazoezi, Pia tunapenda kukaribisha Mandai Herbalist Clinic endapo unasumbuliwa na magonjwa sugu na utapata tiba nzuri kutoka kwa Dk Mandai akishirikiana na timu nzima ya Mandai Herbalist Clinic. Kituo kipo Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaama.

No comments:

Post a Comment