Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 28 February 2015

MCHAI CHAI UNAUWEZO WA KUTIBU MAGONJWA PAMOJA NA KUFUKUZA MMBU
Mchai chai ni kiungo ambacho hutumika kuongeza ladha na harufu nzuri kwenye chai, lakini je unafahamu kuwa kiungo hiki kinaweza kuwa na faida nyingi kwa afya yako.


Tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa mchai chai una vichocheo  muhimu vinavyoweza kupambana na athari mbalimbali tumboni, kwenye mkojo na hata kwenye vidonda. 

Mchai chai pia unatajwa kuwa ni kinywaji kinachoweza kupunguza joto, huku  chai yake ikitajwa kusaidia kupunguza joto kwa mgonjwa wa homa.

Pia chai ya iliyowekwa mchaichai hurahisisha utaratibu wa mmeng’enyo wa chakula, huku ikisaidia sana katika kutibu magonjwa ya kuhara na maumivu ya tumbo ikiwamo tatizo la  kujaa gesi.


Pamoja na hayo, kuna mtatizo ya kiafya ambayo huweza kutatulika kwa kutumia mchaichai, ambayo ni pamoja na tatizo la minyoona kutuliza maumivu ya kiuno na nyonga kwa nyuma.

Pia unapopanda mchai chai nyumbani kwako ni moja ya njia nzuri ya kufukuza mbu, hii ni kutokana na harufu yake na hivyo unapotumia mchai chai utakuwa ukijikinga na ugonjwa wa malaria.


Ikiwa unasumbuliwa na magonjwa sugu unaweza kukutana na Dk Abdallah Mandai sasa na ukapata ufumbuzi wa matatizo yako, kliniki ipo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na inaitwa Mandai Herbal Clinic au unaweza kupiga simu namba  0758 163 818, 0672 060 006, Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment