Monday, 9 February 2015

MIWA PAMOJA NA JUISI YAKE NI TIBA

Kuna baadhi ya vyakula au vinywaji huwa tunapenda kuvitumia sana ingawaje hatufahamu ni nini matokeo yake katika kuboresha afya zetu, miongoni mwa hivyo ni pamoja na hii juisi ya miwa.


Mtaalam wa tiba asili jijini Dar es Salaam, Dk Abdallah Mandai, anasema kuwa, miwa ina faida nyingi katika afya likiwamo hili la uwezo wake mkubwa wa kuupa mwili nguvu kwa sababu ya  'glucose' inayopatikana ndani yake.
Mtaalam huyo, anafafanua kuwa, kjiko kimoja cha juisi ya miwa, kina kiasi cha 'kalori' 11 madini halisi pamoja na vitamin ambazo zinapatikana ni kama 'phosphorus', 'calcium,' madini ya chuma na 'potassium.'

Hata hivyo, Dk Mandai anasema miwa inauwezo mkubwa sana wa kupambana na saratani hususani ile ya kibofu cha mkojo na saratani ya maziwa, uwezo wake huo unaotokana na kuwa miwa ni jamii ya tunda lenye alkali.

Mbali na hayo, virutubisho vilivyopo katika miwa huwa vina manufaa makubwa katika kusaidia utendaji kazi wa ogani muhimu mwilini kama moyo, ubongo, figo na viungo vya uzazi. Hali kadhalika miwa ina upekee wake kwani ina uwezo wa kuongeza maji mwilini na inaupooza mwili na kuupa nguvu.
Picha za mashamba ya miwa

Pamoja na hayo, sukari inayopatikana kwenye miwa ni salama hata kwa wale wagonjwa wa kisukari kwani haina madhara yoyote kwao kutokana na juisi hiyo ya miwa kuwa na sukari halisia.

Tunapenda kukukaribisha Mandai Herbalist Clinic endapo unasumbuliwa na matatizo yoyote ya kiafya yakiwemo magonjwa sugu.Tupo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment