Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 18 February 2015

MLINDE MTOTO WAKO NA KWASHAKOO KWA KUMPATIA VYAKULA VYENYE PROTINI
Kwashakoo ni ile hali ya ukosefu wa chakula chenye protini mwilini, na mara nyingi ugonjwa huu huwasumbua zaidi watoto.


Ugonjwa huu huwapata mara nyingi watoto wenye umri wa mwaka mmoja hadi mitano baada ya kuachishwa kunyonya. 

Dalili ambazo hujitokeza kwa mtoto mwenye ugonjwa huu ni mtoto kudumaa, misuli hunywea, mtoto huwa na huzuni na kupendelea kukaa kimya.

Dalili nyingine ni nywele kubadilika rangi na kuwa laini, rangi ya mwili hukosa damu pamoja na mtoto kuharisha mara kwa mara.

Mtoto mwenye ugonjwa wa Kwashakoo
 
Mtoto mwenye ugonjwa wa Kwashakoo

Mtaalam wa tiba asili Dk Abdallah Mandai anasema kuwa, mtoto anapokuwa na tatizo hili anapaswa kupatiwa maziwa yaliyotolewa mafuta (skimmed milk powder) kama yalivyo kwa kuchanganywa na maji safi na salama au yawekwe kwenye uji wa mahindi na karanga za kusagwa kisha apewe mtoto mara mbili kwa siku.

Aidha, mtaalam huyo anasema mtoto mwenye tatizo hilo pia anaweza kupewa matunda ya aina mbalimbali kama vile papai, embe, machungwa, parachichi, lakini pia naweza kupewa matunda hayo yakiwa yamepondwa kwa kutumia kijiko au akatumia kama juisi.
Vyakula vyenye uwezo wa kuleta protini mwilini


Pamoja na hayo, Dk Mandai anasema ni vizuri pia mgonjwa akapelekwa hospitali au zahanati ili kuweza kupata ushauri na matibabu zaidi.


Unaweza kufika Mandai Herbalist Clinic endapo unasumbuliwa na magonjwa yoyote na hakika utapata tiba nzuri na sahihi na kupona kabisa shida inayokusumbua. Kliniki ipo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.Au piga simu namba, 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com 

No comments:

Post a Comment