Monday, 9 February 2015

MPENDE MTOTO WAKO KWA KUZINGATIA MAMBO HAYA MUHIMU


Wazazi mara nyingi wamekuwa wakishauriwa na wataalam wa afya pamoja na lishe kuwa mtoto mchanga asipewe kitu chochote tangu anapozaliwa hadi afikapo miezi 6, lakini badala yake kwa kipindi chote hicho wazazi hushauriwa mtoto kumpatiwa maziwa ya mama pekee.


Wataalam hao hushauri hivyo kutokana na maziwa ya mama kuwa na virutubisho vyote muhimu vinavyohitajika kwenye ukuaji mzuri wa mtoto na kumpatia kinga ya magonjwa mbalimbali.

Hivyo hii leo Mandai Herbalist Clinic inayofuraha kukufahamisha wewe mzazi namna ya kuanza kumpatia mtoto wako chakula mara anapofika miezi 6 pamoja na faida za lishe bora kwa mtoto wako.

Mtoto anapoanza kupewa vyakula vingine zaidi ya maziwa ni lazima vipondwa vizuri, au viwe kwenye mfumo wa uji au maji sababu mtoto anakuwa hana meno yaliyokomaa na watoto wengine huwa wanakuwa hawajaanza kabisa kuota meno.

Pia inatakiwa kuzingatiwa kuwa, vyakula vya mtoto viwe vya kuongezea lishe, hata hivyo, ni vizuri mtoto akaendelea kunyonya maziwa ya mama hadi atakapofikisha miezi 24.

Hii ni kwa sababu maziwa ya mama ni muhimu katika kumfanya mtoto akue vizuri, hasa katika miezi 24 ya mwanzo.Hivyo endapo hakuna vikwazo vyovyote inashauriwa kuwa mtoto aendelee kunyonya. Vikwazo hivyo vinaweza kuwa ugonjwa wa maambukizi unaoweza kumdhuru mtoto.

Hata hivyo, ni vizuri zaidi mama akimnyonyeshe mtoto kwa muda mrefu zaidi ya miezi sita, kwani kuna faida kubwa za kufanya hivyo kwa mtoto, ambazo ni pamoja na  kumsaidia ubongo wake kukua vizuri zaidi sababu maziwa ya mama yanatoa virutubisho kwa wingi kuliko vyakula atakavyokula yeye moja kwa moja na hii ni kwa sababu kubwa.

Lakini pia ni vizuri ufahamu kuwa tumbo la mtoto huwa halijazoea kusaga vyakula tofauti, hivyo maziwa ya mama ni chakula kinacholeta virutubisho vinavyotumika moja kwa moja mwilini mwa mtoto.

Endapo mtoto atakosa lishe bora basi atakuwa akipata magonjwa mara kwa mara sababu ya kukosa kinga imara dhidi ya magonjwa pia kudumaa kwa akili na mwili.
pamoja na madhara mengine yanayoweza kujitokeza ni uwezekano mkubwa wa kupata ulemavu sababu mifupa kwani inakuwa laini na haiwezi kustahimili uzito wa mwili, hali kadhalika na hata kupata utapiamlo au mtoto kupoteza maisha katika umri mdogo.
Mandai Herbalist Clinic tunapatikana Ukonga, Mongolandege jijini Dar esa Salaam na tunatoa tiba ya magonjwa mbalimbali.

No comments:

Post a Comment