Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 12 February 2015

MWANAMKE AJIFUNGUA MTOTO MWENYE UZITO MKUBWA KIASI CHA KUWASHANGAZA WAUGUZI
Mwanamke mmoja nchini Marekani amejifungua mtoto mwenye uzito mkubwa kuliko ilivyo kawaida na inaelezwa mtoto huyo anakula mara mbili zaidi ya uwezo wa mtoto mchanga.


Mama wa mtoto huyo mwenye kilo 6.4,Bi Maxxzandra Ford amempatia jina la Avery mtoto huyo, na ndiye mtoto mkubwa na mzito kuwahi kuzaliwa katika hospitali ya wanawake ya Mtakatifu Joseph iliyoko Tampa na alizaliwa kwa njia ya kawaida .

Hata hivyo, Ford hakufahamu kuwa ni mjamzito mjamto hadi pale alipotimiza wiki 35, lakini mara baada ya kuwa anaongezeka uzito kupita kiasi, madaktari wakamthibitishia na kugundua kuwa alikuwa ni mjamzito na kutokana na kasi ya unenepaji mwanzo Bi Ford alihisi atajifungua watoto mapacha ingawaje haikuwa hivyo.

Huyu ndio mtoto mkubwa kuliko ilivyokawaida nchni Marekani


Naye Mkunga aitwaye Debbie Moore, kutoka katika hospitali hiyo, alisema endapo wakifahamu mapema kuwa mtoto alikuwa na kilo nyingi kiasi hicho basi kamwe wasingemruhusu mwanamke huyo ajifungue kwa njia ya kawaida.
Pamoja na hayo mtoto huyo Avery bado atabaki hospitalini hapo chini ya uangalizi maalumu tangu alipozaliwa tarehe 29 January , lakini anatarajiwa kuruhusiwa kwenda nyumbani hivi karibuni.

Kabla ya Bi Ford, kujifungua mtoto huyo, hapo awali alikuwa na mtoto mmoja mwenye umri wa mwaka mmoja na mtoto mwingine wa kike mwenye miaka mitano.

Asante kwa kuendelea kutembelea tovuti hii. Pia unaweza kutembelea kituo chetu kiitwacho Mandai Herbalist Clinic kilichopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam endapo unasumbuliwa na magonjwa yoyote.

No comments:

Post a Comment