Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 11 February 2015

MWANZA NDIO MKOA UNAOONGOZA KWA MADUKA YA DAWA BARIDI YASIYOKUWA NA VIGEZO
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif  Rashid amesema mkoa wa Mwanza ndio mkoa ambao umekithili kwa kuwa na maduka ya dawa baridi yasiyokuwa na vigezo wala leseni ya kuuza dawa hizo jambo ambalo linahatarisha maisha ya wananchi wengi.  


Hayo aliyasema juzi wakati wa mkutano na wamiliki wa maduka ya dawa baridi, ambapo Dk Rashid aliwataka watoaji wa huduma hiyo katika mkoa huo kutofungua maduka wala kuuza dawa hizo hadi pale watakapoyabadili maduka yao kuwa ya dawa muhimu ili kulinda usalama wa Watanzania.

Hata hivyo, Dk Rashid alisema kuwa, licha ya mikoa mingine hapa nchini kuuza dawa baridi, lakini Mwanza ni mkoa ambao umeonekana kuwa ni tishio zaidi ya mikoa mingine, jambo ambalo limepelekea kuwepo kwa mvutano kati ya serikali na wamiliki wa maduka hayo.

“Wote ambao watashindwa kufuata utaratibu na sheria hawatavumiliwa, watachukuliwa hatua mapema, mimi niwaombe inabidi mfuate sheria ukishindwa kufuata bora uache kuuza dawa” alisema. 

Naye Mkuu waMkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo alisema kuwa, endapo wataalam hao hawatafuata utaratibu waliokubaliana basi hawatavumiliwa na badala yake watachukuliwa hatua hadi pale  watakapokamilisha utaratibu wa kubadilisha mfumo wa uuzaji wa dawa hizo.

Pamoja na hayo, Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Maduka ya Dawa Baridi  Mkoa (Uwamadamwa ) Robert Nganga, alisema watahakikisha wanafuata utaratibu uliofikiwa kwa lengo la kutoa huduma bora kwa Watanzania.

No comments:

Post a Comment