Tuesday, 24 February 2015

PATA UELEWA KUHUSU KIFUA KIKUU NA TIBA YAKEKifua Kikuu ni ugonjwa ambao huathiri watu wa rika zote na hasa vijana kati ya miaka 15 hadi 44 ambao ndiyo nguvu kazi katika nchi nyingi hapa duniani.


Ugonjwa huu kitaalam hufahamika kama ‘tuberculosis’ na ni ugonjwa ambao unauwezo wa kuenea kwa njia ya hewa, huku ukienezwa na bacteria au kimelea aina ya ‘mycobacterium tuberculosis.’

Mtu anapopata maambukizi ya ugonjwa huu kwa kawaida huathirika mapafu, lakini pia huweza kushambulia viungo vingine vya mwili kama vile tezi za limfu, ubongo na mifupa.

Inapotokea mtu mwenye kifua kikuu, hajaanza tiba anapokohoa, kupiga chafya, kutema mate au makozi, hii huweza kusababisha maambukizi kwa mtu mwingine endapo atavuta hewa yenye vimelea hivyo na kisha kupata ugonjwa huo.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema kuwa kwa mwaka 2013 watu milioni 9 walipata maambukizi ya kifua kikuu, huku watu milioni 1.5 wakifariki dunia.

Pia shirika hilo linaainisha kuwa asilimia 95 ya vifo vitokanavyo na ugonjwa wa kifua kikuu hutokea katika nchi zinazoendelea na zile zenye uchumi wa kati.

Dalili za ugonjwa huu ni kukohoa kwa muda usiopungua wiki mbili na mara nyingine kukohoa damu, homa za jioni za mara kwa mara, kutokwa na jasho usiku, kukosa hamu ya kula, kupungua uzito kwa kiasi kikubwa.

Mgonjwa anayesumbuliwa na Kifua kiuu anashauriwa kula mlo kamili wenye ‘protein’, vitamini na ‘carbohydrate’

Vyakula vyenye protini ni pamoja na mayai, maziwa, maharage na soya. Vyakula hivyo hujenga misuli na kuzalisha chembe za damu. Vilevile husaidia mfumo wa kinga ya mwili kupata nguvu.

Kuna njia mbalimbali za kujikinga na ugonjwa wa kifua kikuu, zipo zile ambazo hutolewa kabla mtu hajapata ugonjwa huo, ambapo chanjo ya kuulinda mwili na ugonjwa huo hutolewa kwa watoto wadogo baada ya kuzaliwa. Chanjo hiyo ya kifua kikuu huitwa BCG.

Kabla ya kuanza tiba ya kifua kikuu ni vizuri kwenda hospitali kwanza na upimwe na kuthibitisha kama ni kifua kikuu, lakini pia unaweza kutumia kitunguu swaumu kama tiba ya ugonjwa huu.


Pondaponda punje 18 za kitunguu swaumu, kisha loweka ndani ya glasi ya maji na uongeze vijiko vitatu vya mezani vya asili kisha koroga vizuri.

Baada ya hapo gawanya mchanganyiko huo katika sehemu tatu zinazolingana na unywe mara tatu kwa siku na uendelee na tiba hiyo kwa muda wa miezi miwili na wakati unaendellea na tiba hii ikiwa ukahisi maumivu kifuani na hali ya kichomi, sugua kitunguu swaumu kilichopondwa katika sehemu zote za maumivu.

Sasa tupo tayari kuanza kupokea matangazo ya biashara yako yoyote na kukuwekea kwenye tovuti hii inayotembelewa na maelfu ya watu. Karibu sana gharama zetu ni nafuu sana piga simu namba 0758 163 818, 0672 060 006, Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment