Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 5 February 2015

SABABU ZINAZOCHANGIA KUTOKA KWA HARUFU MBAYA SEHEMU ZA SIRI KWA WANAWAKEKutokwa kwa harufu mbaya ni moja ya tatizo linalowasumbua na kuwakwaza wanawake wengi. Kitaalamu hali ya mwanamke kutokwa na majimaji yenye rangi nyeupe au ya njano ni hali ya kawaida na wala siyo tatizo, lakini endapo maji hayo siyo mazito sana na wala hayatoi harufu mbaya.

Mtaalam wa tiba asili Dk Abdallah Mandai, anasema kuwa kutoka kwa majimaji au ute unaoteleza kutoka sehemu za siri ni njia mojawapo ya asili ya viungo vya uzazi vya mwanamke kujisafisha na kuutoa uchafu wa seli zilizokufa na mabaki ya damu ya hedhi nje ya mwili.

Mtaalam huyo anasema zoezi hilo pia husaidi kuvikinga viungo vya uzazi vya mwanamke dhidi ya maambukizi ya fangasi au bacteria walinaosababisha magonjwa, lakini kwa kawaida majimaji hayo huwa hayatoi harufu na huwa na rangi nyeupe au ya njano.

Kwa kawaida, mwanamke hutoa ute mwepesi kila siku na hii hutegemeana na mzunguko wa hedhi, kwani kuna kipindi ute huo huwa mwepesi na unaovutika, lakini pia wakati mwingine huwa mzito kiasi na wenye rangi ya njano. Yote hayo ni ya kawaida na hutokea kwa wanawake hususani wale waliokwisha vunja ungo.

Dk Mandai anasema sababu ya kutoka kwa ute au majimaji yasiyo ya
kawaida kwenye sehemu za siri za mwanamke ni maambukizi ya bacteria wanaosababisha magonjwa kama vile candidiasi, gonorrhea au uambukizo wa Candida alb cans.

Aidha, Dk Mandai anabainisha kuwa, pia tatizo hili huweza kuchangiwa na uwepo wa mabaki ya pedi au tissue ambazo hutumika wakati wa kipindi cha hedhi. Pia usafi unapokosekana wakati wa kipindi cha hedhi huweza kuchangia sehemu za siri za mwanamke kutoa harufu mbaya pia.

Pamoja na hayo, Dk Mandai anasema kuwa dalili za tatizo hili ni pamoja na kuwashwa sana sehemu za siri, maumivu makali wakati wa tendo la ndoa, mwanamke anatokwa ute uliochanganyikana na damu hata kama hayupo kwenye siku zake.

Dk Mandai anasema ni vizuri kuwahi kuwaona wataalam wa afya mara tu unapoona dalili za tatizo hili na ukafanyiwa vipimo zaidi na ukigundulika unatatizo unaweza kupatiwa dawa za kupaka au dawa za kumeza pia ili kumaliza tatizo hilo.

Pia unaweza kufika Mandai Herbalist Clinic nakupata tiba ya magonjwa mbalimbali likiwemo tatizo hili, kituo kipo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment