Tuesday, 24 February 2015

SERA MPYA YA MATUMIZI YA SINDANO IMEZINDULIWAShirika la Afya Duniani, WHO, limezindua sera mpya inayopendekeza matumizi ya bomba la sindano na sindano za kisasa na salama zaidi, ili kuzuia maambukizi ya magonjwa.


Kwa mujibu wa WHO, zaidi ya watu milioni mbili duniani wameambukizwa magonjwa kama vile homa ya Ini na virusi vya UKIMWI kupitia sindano zisizokuwa salama.
Kawaida bomba la sindano na sindano yake hupaswa kutupwa mara baada ya kutumiwa mara moja tu, lakini watu wengi hasa katika nchi zinazoendelea hutumia kwa zaidi ya mara moja.

Sera hiyo mpya inataka sindano isiyoweza kutumika zaidi ya mara moja na ambayo inajiharibu yenyewe mara baada ya kutumiwa.

Edward Kelley ni Mkurungenzi wa Idara ya Usalama, WHO, amesema wanaamini teknolojia hiyo mpya itatumiwa kote duniani ifikapo mwaka 2020.

"Tatizo la sindano zisizokuwa salama si jipya. Lakini kitu kipya sasa na matumaini mapya siku za usoni ni matumizi ya masharti salama pamoja na teknolojia njema kwa ajili ya mfumo salama wa afya."

No comments:

Post a Comment