Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 18 February 2015

SHIRIKA LA AFYA DUNIANI LIMETOA TAKWIMU MPYA KUHUSU VIFO VILIVYOTOKANA NA EBOLA
Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa takwimu mpya kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.


Takwimu hizo zinazihusu nchi za Sierra Leone, Guinea na Liberia tu, ambapo taarifa zinasema kumekuwa na wagonjwa 23 218 na vifo 9365.

Mchanganuo wa takwimu hizo unaonesha kuwa Sierra Leone imekuwa na wagonjwa 11 103, na vifo vya watu 3408, Liberia, wagonjwa 9007 na vifo 3900 na Guinea, wagonjwa 3108 na vifo vya watu 2057.


Takwimu hizi ni mpaka tarehe 15 Februari kwa nchi za Sierra Leone na Guinea, na Liberia ni mpaka tarehe 12 Februari.

Mbali na nchi hizo, pia Uingereza ilikuwa na mgonjwa mmoja bila kifo

Pamoja na hayo, takwimu kwa ajili ya Senegal, Nigeria, Hispania, Marekani na Mali zimeondolewa.Nchi hizo haziko katika karantini ya ugonjwa wa Ebola.

No comments:

Post a Comment