Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 17 February 2015

TATIZO LA MIMBA KUTUNGA NJE YA KIZAZI HUTESA WANAWAKE, FAHAMU DALILI ZAKEBaada ya jana kuzungumzia tatizo la mimba kutunga nje ya kizazi, ni vizuri leo tufahamishane dalili za tatizo hilo.


Dalili za tatizo hili mara nyingi huanza kujitokeza kati ya wiki sita hadi nane baada ya mwanamke kuona hedhi kwa mara ya mwisho.

Hata hivyo, mwanzoni mwa ujauzito hususani katika wiki ya kwanza, mimba iliyotunga nje ya mfuko wa kizazi huwa na dalili sawa na zile za mimba iliyotungwa eneo la kawaida.

Hivyo ni vigumu kujua mimba iliyotungwa nje ya mfuko, licha ya kuwa inaweza kuchochea kupata kichefuchefu na kuishiwa nguvu, lakini dalili hizi piahuweza kuwapata pia wale ambao mimba zimetungwa eneo la kawaida.

Mara zote huwa inashauriwa mama mjamzito kwenda kliniki mapema angalau katika kipindi kisichozidi miezi mitatu, na ikiwa atabainika kuwa na shida hiyo aweze kuhudumiwa.

Mama anapochelewa hadi mimba ikafikia miezi sita hadi nane, huwa tayari mirija ya uzazi imeshazidiwa na hivyo kushindwa kuhimili kuubeba ujauzito, hivyo humfanya mwanamke kupata maumivu makali chini ya nyonga, kuhisi kizunguzungu,shikizo la damu kushuka na damu kutoka ukeni.

Maumivu huwa ni makali sana kwa mwanamke mfano wa kisu kinapokata na yanaweza kuwa ni ya upande mmoja wa nyonga .

Tatizo hili huweza kutibiwa kwa namna mbili,yaani upasuaji au kutumia dawa, lakini endapo mirija itakuwa tayari imeshapasuka basi upasuaji wa dharura hufanyika kwa ajili ya kuzuia kupoteza kwa damu zaidi.

Unaweza kufika Mandai Herbalist Clinic endapo unasumbuliwa na magonjwa yoyote na hakika utapata tiba nzuri na sahihi na kupona kabisa shida inayokusumbua. Kliniki ipo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.Au piga simu namba, 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment