Wednesday, 4 February 2015

TATIZO LA UGUMBA KWA WANAWAKETatizo la ugumba kwa wanawake ni moja ya tatizo ambalo huwakabili watu wengi na hata kuwasababishia kukosa amani na furaha ndani ya familia zao, na mara nyingine hupelekea familia/ ndoa kuvunjika kabisa.

Sababu kubwa ya wanawake kutopata mimba ni pale ambapo mayai yanapokuwa hayajakomaa vizuri, hivyo kufanya mwanamke kushindwa kushika ujauzito.


Hali hiyo huchukua karibu asilimia 30 ya wanawake wote wagumba. Habari njema ni kwamba tatizo hili linaweza kurekebishwa kirahisi ikiwa mwili utapewa vile viini lishe muhimu vinavyokosekana hadi kupelekea kusababisha mayai kutokomaa vizuri.

Aidha, mambo yanayosababisha mayai kushindwa kukomaa vizuri ni pale mwanamke anapokuwa na matatizo katika homoni, hii ni kwa sababu hatua za kukomaa kwa mayai hutegemea uwiano mzuri wa homoni na namna zinvyotegemeana katika kufanya kazi.


Jambo lolote linalosababisha mvurugiko wa homoni na kusababisha kutobaki katika uwiano na wenye kufanya kazi ipasavyo linaweza kusababisha utungaji wa mayai ambayo hayajakomaa vizuri. Matatizo haya katika homoni hutokana na ufanyaji kazi usioridhisha wa hypothalamus.

Hypothalamus ni sehemu ya mbele ya ya ubongo ambayo inajukumu la kutuma ishara (signals) kwenda katika tezi ya pituitary ambayo yenyewe tena hutumia uchochezi wa kihomoni  kwenda kwenye ovari katika mfumo wa F.S.H  ili kuanzisha ukomaaji wa mayai.

Ikiwa hypothalamus inashindwa kufanya kazi zake vizuri kutungwa kwa mayai ambayo hayajakomaa ndiyo kutakuwa ni matokeo yake. Hali kadhalika tatizo hili husababishwa na ufanyaji kazi usioridhisha wa tezi ya pituitary. Muendelezo wa makala hii utaupata kupitia Gazeti la Ijumaa Wikienda............, lakini unaweza kufika Mandai Herbalist Clinic kituo kilichopo Ukonga Mongalendege jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment