Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 25 February 2015

TATIZO LA UPUNGUFU WA DAMU (ANEMIA) SEHEMU YA 2Baada ya kufahamu kuhusu tatizo la upungufu wa damu mwilini (anemia) leo tufahamu kuhusu aina mbalimbali za tatizo hilo.


Miongoni mwa aina za tatizo hili ni pamoja na hii ya iron defiency anaemia, huu ni upungufu wa damu anaopata mtu wakati anapopoteza kiwango fulani cha madini ya chuma mwilini. 

Kwa kawaida mwili wa mwanadamu huhitaji madini ya chuma ili kuweza kuzalisha chembe nyekundu za damu na inapotokea mtu akapoteza  kiasi fulani cha damu basi madini ya chuma nayo hupungua mwilini na hivyo kusababisha upungufu wa madini hayo kwa muda.

Aina nyingine ya upungufu wa damu ni 'hemolytic anemia,' aina hii ya chembe nyekundu za damu huharibiwa haraka kuliko mwili unavyoweza kuzalisha chembe nyingine.
Upungufu huu husababishwa na mambo mengi lakini miongoni mwa sababu hizo ni pamoja na saratani aina ya ‘lymphoma’
Pia aina nyingine ni ile ya pernicious anemia. Huu ni upungufu wa damu unaotokana na ukosefu wa kutosha wa acidi aina ya folic (foliate) katika chakula.

Folate hupatikana katika mbogamboga za majani, matunda na nyama.
Aina nyingine ni aplastica anemia. Huu ni upungufu wa damu unaotokea wakati ‘bone marrow’ zinaposhindwa kuzalisha chembe nyekundu za damu ipasavyo. Baadhi ya upungufu huu wa damu humpata mtu anapotumia tiba ya miale (radio therapy) au dawa za saratani na kemikali nyinginezo.

Sickle cell ni aina nyingine pia ya tatizo la upungufu wa damu mwilini, hii inatokea pale ambapo chembe nyekundu za damu huwa na muundo usio wa kawaida unaozuia na kuathiri mishipa midogo ya damu na hivyo kusababisha kuziba kwa mishipa hiyo ya damu na hata kiungo cha mwili. 

Kwa msingi huo ni muhimu kwa mtu kujua aina ipi ya upungufu wa damu aliyonayona na hilo hujulikana baada ya daktari kukuandikia vipimo kadhaa vya damu ambavyo vitaonesha unakabiliwa na aina ipi ya anemia. 

 Sasa tupo tayari kuanza kupokea matangazo ya biashara yako yoyote na kukuwekea kwenye tovuti hii inayotembelewa na maelfu ya watu. Karibu sana gharama zetu ni nafuu sana piga simu namba 0758 163 818, 0672 060 006, Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment