Saturday, 28 February 2015

TUMIA MIZIZI YA MPAPAI KAMA DAWA YA MARADHI MENGI LIKIWEMO HILI TATIZO LA FIGO
Papai ni moja ya tunda linalotumiwa na watu wengi hapa nchini, lakini pamoja na kutumiwa huko wengi wao hawafahamu namna tunda hili linavyoweza kuwa tiba ya maradhi mbalimbali.


Kutoka kwetu Mandai Herbal Clinic leo hii tunakufahamisha manufaa ya kula tunda hili na faida zake kiujumla katika masuala ya tiba.

Mizizi ya mpapai inapochemshwa huweza kutumika kama dawa ya figo zinazovuja, kuua minyoo tumboni pamoja na kutibu meno hususani pale inapochanganywa na miche mingine.

Pia mizizi ya mpapai inapopondwa na kulowekwa katika maji yaliyochemshwa husaidia sana kutibu matatizo ya figo na kibofu pamoja na kuzuia kutapika.Mbali na tiba hizo, pia majani ya mpapai husaidia kutibu tatizo la pumu sambamba na tatizo la shinikizo la damu.

Hayo ni machache tu kuhusu tiba ya mpapai, lakini unaweza kuendelea kuwa karibu na tovuti hii ili ufahamu mengi zaidi juu yam mea huu wa mpapi katika tiba, lakini endapo unasumbuliwa na magonjwa sugu basi unaweza kufika Mandai Herbal Clinic kituo kilichopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na utaonana na Dk Abdallaha Mandai na hakika utapata tiba sahihi.

Pia unaweza kuwasiliana na Mandai Herbal Clinic kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.   

No comments:

Post a Comment