Thursday, 19 February 2015

UGONJWA WA KIFAFA WASABABISHA JAMAA KUKOSA MKE.
Kuna ule usemi usemao bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi basi kauli hiyo ilidhibitika kwenye harusi moja huko kaskazini mwa nchini India.


Hii ni baada ya bi harusi mmoja kaskazini mwa nchi hiyo, kufanya maamuzi ya papo kwa hapo na kuamua kuolewa na mmoja wa wageni waliofika kushereheka naye katika harusi yake baada ya mumewe kuugua ghafla ugonjwa wa kifafa wakati wa harusi yao.

Taarifa zinasema kwamba mwanamke huyo ajulikanaye kama Indra na anatokea Rampur jimbo la Uttar Pradesh, ambapo ilielezwa kuwa sekunde chache kabla ya ndoa ya wawili hao mume alianguka kifafa, na hivyo kumlazimu kuondoka harusini na kwenda kumuona daktari.

Hata hivyo, kufuatia tukio hilo, bi harusi Indra, alishikwa na hasira ya hali ya juu, kwakuwa mume wake huyo alimficha juu ya hali yake hiyo, naye hakuwahi kujua hata siku moja kuwa , jamaa ana tatizo la kuanguka kifafa.

Pia hasira za mwanamke huyo zilienda mbali zaidi na kuamua kutoa ombi lake kuwa anahitaji kuolewa na mmoja wa wana familia ya bwana harusi, ambaye alikuja harusini kusherehekea harusi ya nduguye, na Indra akamtaka achukue nafasi ya nduguye badala yake.

Ombi la mwanamke huyo Indra halikupata vikwazo vyovyote na baadaye mmoja wa ndugu wa mume alikubali na ndoa ikafungwa, huku  hali ya bwana harusi wa kwanza mwenye kuanguka kifafa, haijajulikana mpaka harusi ya pili ilipokwisha.

Story hii inatufunza kujenga tabia ya kuwa wawazi na wakweli kwa watu wetu wa karibu juu ya afya zetu na maisha yetu kwa ujumla ili kuepukana na matukio kama haya.

BBC


No comments:

Post a Comment